MAMLAKA YA MAPATO ZANZIBAR ( ZRA) YAWATOA HOFU WANANCHI JUU YA KODI YA MAJENGO ZANZIBAR.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA.
MAMLAKA ya mapato Zanzibar ( ZRA ) Imewatoa hofu wananchi kuhusu maneno ya upotoshaji yanayoendelea kutolewa na baadhi ya wananchi wasiopenda maendeleo juu ya ukusanayaji wa kodi ya majengo ambapo imesema kodi hiyo haitowahusu wamiliki wa nyumba za kawaida za makazi kama inavyosambazwa na baadhi ya watu wachache wasio na uelewa.
Akizungumza na viongozi wa mkoa kusini na kaskazini Pemba Kamshina mkuu wa mamlaka hiyo Zanzibar Yussuf Juma Mwenda amesema kuwa majengo ya ghorofa yanayofanyiwa biashara pekee ndio ambayo yatahusika na kodi hiyo ambayo pia haitowaumiza wamiliki wake kutokana na unafuu uliowekwa.
"Mitaani kuna maneno uko lakini ukweli haupo ivyo unavyosemwa mitaani, ukweli ni kuwa kodi hii sio ya wote bali ni ya watu wachache ambao wanamiliki majengo ya ghorofa".
Na wao pia haitowaumiza hiyo kodi kwa sababu ni yenye unafuu mno ni kodi ambayo kwa mwaka kila mmiliki atalazimika kulipa shilingi 10000 tu ambayo kwa mwezi ni sawa na shilingi 830 lengo ni kuongeza makusanyo kupitia vyanzo mbali mbali kwalengo la kuleta maendeleo ". Alisema.
Aidha Mwenda amesema kuwa Serikali ya Zanzibar inayoongozwa na Dk Hussein Ali Mwinyi katika kuhakikisha inarahisisha maisha bora kwa wananchi wake imeamua kutokuziingiza nyumba za kawaida katika kodi ya majengo kama zilivyo katika nchi nyengine.
"Mh Rais Katika kuwajali wananchi wake ametutaka nyumba za kawaida za wananchi tusiziweke katika kodi hii ya majengo, akatutaka pia hizo kodi katika hayo majengo zisiwaumize wananchi hakuna popote ambapo jengo linalipiwa gharama hiyo kwa mwezi isipokuwa Zanzibar ".
Aidha kamishna amewataka viongozi wa shehia wilaya na mikoa kuwasaidia kuyatambua majengo hayo pamoja na wamiliki wake ambayo yamo katika shehia zao sambamba na kutoa elimu sahihi kwa wananchi juu ya ulipaji kodi ya majengo.
Akizungumza katika mkutano huo Mkurugenzi ZRA Pemba Jamal Hassan Jamal amesema lengo la kurudishwa upya kodi hiyo ni katika kuleta maendeleo kwa wananchi ikiwemo kuboresha miundo mbinu afya pamoja na elimu ambao kodi hizo zinazokusanywa na mamlaka hiyo hutumika kwa matumizi mbali mbali ya wananchi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mikutano hiyo mkuu wa mkoa wa Kaskazini na Kusini Pemba Salama Mbarouk Khatib Pamoja na Mattar Zahor Massoud wamesema wataendelea kuiunga mkono serikali katika kushajihisha zaidi ukusanyaji wa kodi mbali mbali ili kuweza kupanga zaidi mipango ya maendeleo.
Kodi ya majengo Zanzibar imeanzishwa kwa mujibu wa Sheria namba 14 mwaka 2008 lengo ikiwa ni kuongeza vyanzo vya mapato ya kukusanya kodi Zanzibar Ambapo mikutano hiyo maalum iliyoandaliwa na mamlaka hiyo katika ukumbi wa Baraza la wawakilishi Wete Upande wa kaskazini sambamba na Baraza la Manispaa Chake Chake ambao viongozi wa shehia na viongozi mbali mbali walishiriki katika mkutano huo.
.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment