WANAFUNZI TOENI TAARIFA MKIONA VIASHIRIA VYA UDHALILISHAJI

NA, IS-HAK MUHAMED, PEMBA. 

WANAFUNZI wa Skuli za Mwambe za Dkt. Samia Suluhu Hassan Sec, Dkt. Hussein Mwinyi Msingi na Mwambe Msingi wamehimizwa juu ya muhimu ya kutoa taarifa pale wanapokubwa na changamoto mbali mbali zikiwemo za viashiria vya vitendo vya kufanyiwa uzalilishaji wa kijinsia.


Wito huo umetolewa na Mratibu wa Chama cha Waandishi Wanawake Tanzania, Zanzibar Tamwa Fat-hiya Mussa Said wakati akiwasilisha mada juu ya Changamoto zinazowakabili watoto katika mafunzo yaliyoandaliwa na Shirika la Save the Children na kuwajumuisha wanafunzi wa Skuli hizo.

Amesema zipo changamoto nyingi zinazowakumba watoto ikiwemo unyanyasaji wa kijinsia, kimwili, kingono, kutekelezwa na nyengine nyingi lakini watoto hao wamekuwa wakishindwa kuziripoti jambo ambalo husababisha wafanyaji kuendelea na vitendo hivyo wakitambua kuwa hawaulizwi.

Kwa upande wake Afisa Mradi Jumuishi katika Shirika la Msaada kwa watoto la Save the Children John Maftah amesema pamoja na jamii kuendelea kufanya utetezi wa haki za watoto wazingatie pia katika utetezi wa haki ya mtoto wa kike ambazo kwa kipindi kirefu haki zao zilikuwa hazipewi kipaumbele.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI