Wanafunzi wafunzwa kutumia zoom, kuwasiliana na viongozi
NA IS-HAKA RUBEA, PEMBA.
KUWEPO kwa jukwaa la kuwasiliana mtandaoni kumeelezwa kutawasaidia watoto katika kuwasilisha changamoto zao ili ziweze kuchukuliwa hatua kwa haraka na walengwa ikiwemo masuala yao ya kudai haki zao za kimsingi.
Hayo wameyaeleza wanafunzi wa Skuli za Samia Suluhu Hassan na Mwambe Wilaya ya Mkoani Pemba, wakati wakizungumzia mafunzo ya kuwasiliana Mtandaoni(Zoom Meteeng) yaliyotolewa na Shirika la Save Tha Chidren Tanzania kwa wanafunzi hao ikiwa ni katika kujenga jukwaa la kuwasiliasha maoni ya watoto kupitia mikutano ya Mtandaoni.
WaKizungumza baadhi ya wanafunzi hao wamesema kuwa kupitia kupitia njia hiyo ya matumizi ya mtandao itakuwa rais kwao kama watoto kuweza kuwasilisha maoni yao mbali mbali ikiwemo yale ya kudai haki kwa mamlaka za juu ambao kuwapata kukaa maza moja inaweza kuwa shida kwa wanafunzi na watoto wengine.
Mratibu wa Mradi wa Kulinda na kutetea Haki za mtoto kupitia shirika la Save the Childen Unguja Pius Ulaya amesema teknojia ya mtandao endapo itatumika vyema itawawezesha watoto kuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na viongozi wao ili kuwasilisha madai juu ya haki zao ambazo zinakosekana.
Kwa upande wake Mratibu wa Mradi huo Pemba Micheal Mwalupale amesema kupitia fursa za kujieleza kwa watoto hao kwa viongozi wenye mamlaka itakuwa rahisi kwa watoto hao kuzipata haki zao kwa urahisi na kwa wakati.
Comments
Post a Comment