ZRA KUDHAMINI MGENI NDONDO CUP MSIMU UJAO WAASWA KUHAMISHA ULIPAJI KODI NA MATUMIZI YA RISITI ZA KIELECTRONIKI.
NA, AMINA AHMED MOHD, PEMBA.
KATIKA kuhamasisha ulipaji wa kodi, kudai risiti za kielectroniki wakati wa kununua bidhaa katika maduka mbali mbali Kamishna wa mamlaka ya mapato Zanzibar ZRA Yussuf Juma Mwenda akiambatana na wasaidizi wa mamlaka hiyo wamefika katika uwanja wa shaame mata Wilaya ya Micheweni kuzungumza na wadau wa mpira wa miguu kutoa elimu juu ya suala hilo.
Kamishna mwenda amewataka wanamichezo kuendelea kuisaidia serikali suala la risiti za kielectroniki pamoja na ulipaji kodi ili kuendeleza shughuli mbali mbali za maendeleo ikiwemo uimarishaji wa viwanja vya michezo.
Sisi Peke yetu bila mashirikiano hatutweza kuishinda hii vita kila mmoja wetu kwa nafasi yake akumbuke kuwa wajibu wake ni kusaodia serikali juu ya suala zima la kodi.
Aidha kamishna ameahidi udhamini wa mashindano ya kombe la Mgeni ndondo cup linalowakutanisha vijana wa michezo katika wilaya ya micheweni pamoja na wilaya jirani katika msimu ujao wa mashindano hayo ikiwa ni sehemu ya kuongeza nguvu katika kuuinua michezo wilayani humo kupitia kodi zinazokusanywa na mamlaka hiyo.
Comments
Post a Comment