Tutaendela kudhibiti utoro wa skuli za msingi
Na AMINA AHMED MOH’D - PEMBA Uongozi wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kaskazini Pemba Umesema utaendelea kulisimamia vyema suala la utoro wa wanafunzi wa skuli za msingi kwa kuendelea kukemea ajira za watoto wilayani humo ili lisiendelee kujitokeza na kuathiri maendeleo ya elimu kwa watoto na kupelekea kukosa haki yao ya msingi kwa kukatisha masomo Ameyasema Hayo Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni khatib Yahya Alipokuwa akizungumza na habari hizi juu ya maendeleo yaliofikiwa katika kuwarejesha skuli wanafunzi watoro wa skuli za msingi zilizomo katika skuli mbali mbali za wilaya hiyo. Amesema moja kati ya sababu iliyopelekea kuwepo kwa utoro wa wanafunzi wa skuli za msingi ktika baadhi ya skuli wilayani humo ni pamoja na ajira za watoto pamoja kukosa mashirikiano kwa waza jambo ambalo kwa sasa limepunguwa baada ya kuliwekea mikakati maalum. "Tatizo kubwa la utoro kwa wanafunzi wa skuli za msingi Waka...