Teknologia ya Habari kuzidi kuimarika Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ukamilikaji wa ujenzi wa minara 42 ya mawasiliano na vituo 11 vya Teknolojia, Habari,  Mawasiliano (TEHAMA) imefungua ukarasa mpya wa mawasiliano Zanzibar.
 
Ameyasema hayo leo mara baada ya kufungua kituo Cha TEHAMA kilichojengwa kupitia mfuko wa mawasiliano kwa wote (UCSAF) kilichopo Bwefum Mkoa wa Mjini Magharibi.
 
Pia, Rais Dk.Mwinyi amezindua mnara wa mawasiliano uliojengwa Kisakasaka wilaya ya Magharibi 'B'.
 
Rais Dk.Mwinyi  amesema kukamilika kwa vituo hivyo vitasaidia kuchochea ukuaji wa matumizi ya TEHAMA ambayo wananchi wengi watatumia kwenye shughuli za kila siku.
 
Amesema kukamilika kwa ujenzi wa minara hiyo 42 itaondoa malalamiko ya wananchi katika ukosefu wa huduma ya mawasiliano pamoja na kuwepo kwa hali ya usalama na mali za wananchi pamoja na wageni wanaoingia Zanzibar. 

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.