HALI ZA WAGONJWA WANAODAIWA KULA SAMAKI AINA YA BUNJU ZINAENDELEA VIZURI.
Na AMINA AHMED MOH’D -PEMBA
Uongozi wa Hospitali ya Cottage Micheweni Imesema Hali ya Majeruhi waliolazwa wanaodaiwa kula chakula cha baharini samaki kinachodaiwa kuwa na sumu zinaendelea vizuri sambamba na kuendelea vyema kupatiwa huduma za mtibabu ili hali zao ziweze kurejea kama zilivyokuwa awali .
Akizungumza na habari hizi Daktari dhamana hospitali ya Micheweni Cottage Ali Hamad Sharif amesema kuwa mpka sasa Hali zinaendelea vizuri licha ya kuwa bado Haijajulikana Rasmi aina ya chakula na samaki waliokula Watu saba wa familia moja hiyo na kupata madhara hayo kutokana na wahusika wenyewe kutoa taarifa za tofauti.
Hali zao mpka sasa zinaendelea vizuri Kwa. sababu wapo ambao alikuja hawawezi kula lakini sasa wanaweza na huduma za matibabu zinaendelea ila bado Hatujathibitisha nakujua ni aina gani ya samaki wamekula hatujajua bado ni bunju au ni kasa kwa vile wanatoa maelezo tofauti tofauti mara wanasema wamekula samaki mara wamekula maini ya samaki kwaio tunaendelea na chunguzi kujua ni aina gani .
Alisema kuwa wagonjwa hao walifikishwa hospitali hapo mnamo majira ya saa moja za usiku wa kuamkia leo baada ya kuhofia kula na uhisi mabadiliko ya afya zao tangia Saa saba za mchana.
" Tumewapokea Wagonjwa hawa saa moja na nusu za usiku walipata dalili za kizungu zungu, kutapika, na wakajitafutia huduma ya mwazo wakiwa majumbani mwao na katika hao watu saba walikuwa wanawake wawili na wanaume watano wote wa familia moja baba mama na watoto wake".
Daktari huyo Aliendelea kusema kuwa Licha ya hali za wagonjwa hao kuendelea vizuri lakini wapo ambao kati yao hali zao bado hazijatengamaa vyema kutokana na wengine hao kufika hospitali hapo wakiwa tayari wameishiwa nguvu kutokana na kutapika sana pamoja na kulalamika kuumwa na viungo.
Awali akizungumza Baba Mdogo wa Familia hiyo alisema Alikuta tayari wamekula chakula pamoja na kitoleo ambacho kiliwafanyia matatizo na kuhofia baada ya mmoja wao kuhisi kizungu zungu mda mchache baada ya kumaliza kula jambo ambalo lilikuwa likiendelea kwa wanafamilia wote.
" Walianza kushuku utowezi waliokula baada ya kuhisi kizungu zungu, na Baba yao kutilia hofu lakini wasi wasi zaidi ulikuja baada ya kuona zile miba wlizokula wakazitupa kuku wadogo ambao walidona dona na wao walikufa pale pale baada ya kula zile miba."
Aidha aliendelea kusema samaki aina ya bunju hutumika kama kitoweleo chengine jambo ambalo halikuwatia hofu wanafamilia hiyo katika kukitumia kitoleo hicho.
" Walikula kwa kujua ndio kwa sababu ni samaki kama kitoleo chengine ndio jina lake bunju ila sio kwamba walijua kama atakuwa na atahari kwa vile ni kitoleo cha kawaida na siku nyingi leo tu labda imetokezea mistake labada kal kitu labda kala kitu cha sumu labada ayo maini yake yalikuwa ni machafu ndio wakadhurika.
Akizungumza kwa upande wake Baba Mzazi wa Familia hiyo Alisema Alipata samaki hao bandarini alipokuwa katika harakati zake za kutafuta kitoleo Kwa Ajili ya Matumizi Ya Nyumbani Kwake.
"Nilipata Maini yale, Machali Chali, Vichwa Vidogo Vidogo Vya Bunju Lakini Baada ya kulikuta lile lishachunwa vizuri nikalichukua Sikuhofia kwa sababu nishakula siku nyingi tu mambo kama hayo si chini ya miaka Lakini ni mtihani tu mwenyezimungu mja akishakuandikia lolote linakuwa,
Hata hivyo Daktari huyo aliwataka wananchi kutoendelea kutumia samaki ambao tayari wanahofu kutokana na kuwa na vinasaba amabavyo vina atahari kwa binaadamu ili kuepusha Kuhatarisha usalama wa maisha yao.
"Mara kwa mara kesi za ulaji wa samaki hawa amabao wanavinasaba vyenye sumu mbaya endapo atatumia binaadamu zinajitokeza wananchi waache kula ni hatari kwao".
Kwa Mujibu wa Dakatari huyo dhamana alissema Wanafamilia hao mmoja kati yao amepoteza maisha usiku wa saa tisa mtoto mwenye umri wa miaka 5.
"Familia hiyo inatokea shehia ya tumbe Magharibi kikunguni Mtaa wa Soko domo, na Said Omar Kassim amabae ni baba wa familia hiyo Hali yake Bado anaendelea na matibabu licha ya kulalamika mara kwa mara kizungu zungu, Jine Issa Abdalla Ambae ni mama wa familia hiyo yenye watoto watano umri miaka 37 hali yake inaendelea vizuri, Abdul Majid Said Omar, Issa Said Omar, Hassan Said Omar, Muzna Said Omar, wote Wanaendelea na matibabu hospitalini hapo huku Shafii Saidi Omar Akiwa tayari amepoteza Maisha mwenye umri wa miaka 5 .
Familia hiyo inaendelea kupata matibabu katika hospital ya Cottage Micheweni ambapo Imefikishwa hospitlini hapo kwa kudaiwa kula samaki aina ya bunj
Comments
Post a Comment