WAATHIRIKA WAKUBWA UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI NI AKINA MAMA BAADHI YA VIJIJI WALIA KUKOSA HUDUMA.
Na AMINA AHMED MOH’D
Wananchi wanalalamika kukosa huduma ya maji safi na salama kwa muda wa miezi mitatu sasa licha ya kufika mmlaka husikakuomba msaada wa kupatiwa ufumbuzi suala hilo.
Wakizungumza baadhi ya kina mama katika kijiji cha kichanjaani shehia ya Dodo Pujini wilaya ya mkoani mkoa wa kusini pemba wamesema kukosa huduma hiyo kwa kipindi cha miezi mitatu kumekuwa usumbufu jambo ambalo hulazimika kusitisha baadhi y shughuli zao ikiwemo kilimo .
Akina mama hao wameiomba serikali pamoja na viongozi wao wa jimbo kuwasaidia kulipatia ufumbuzi suala hilo ambapo wamesema licha ya kukosa huduma hiyo kwa ajili y shughuli zao lakini pia husababishia usumbufu wa kuifata masafa ya mbali huduma hiyo.
" Tunaiomba serikali ituangalie wananchi wake tunasumbuka vikuta vya mifereji vimeshakauka maji tukikosa kupeleka dumu mbili mbli hapa kwenye kisima hichi cha Msikiti bhasi ndoo hatujsalimika na kichwani kil siku Alisema Mastura Ali Mkaazi wa kichanjaani.
Aidha kwa upande wake Fatma Salum Amesema kuwa kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu sasa hulazimika kusitisha huduma za kilimo.
"Maji tumekuwa sikuizi hatulimi hata mboga mana ndo htuna maji kukosa mji kila kiu kimekuwa kigumu mana shughuli za kiuchumia zimesimama kil kitu tununue mpka majani y mboga"
"Tunayafata mabondeni maji sisi na watoto wetu visimani hatari kama nini dunia hii iliyojaa udhalilishaji wkati mwengine watoto wakike wanaenda peke yao kufuata maji Viongozi tusaidieni maji ndio kila kitu kwa binaadamu Alisema Bi suria Juma."
Kwa upande wa akina baba kijijini humo wamesema kuwa wamekuwa wakichukua hatua mbali mbali kulipatia ufumbuzi sul hilo ikiwa ni pamoja na kufika mamlaka husika kuomba usaidizi juu ya suala hili linalowakbili kijijini humu".
Akizungumzia suala hili sheha wa shehia ya Dodo Pujini Ramadhan Farhan Farjala amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika badhi ya meneo ndani ya shehia yake ambapo amesema uongozi wa shehia umechukua jitihada mbali mbali ikiwemo kulipfikisha suala hili katika uongozi wa wilaya.
"Ni kweli vijiji vitatu katika shehia ya Dodo Havina huduma ya mji miezi mitatu sasa Chanjaani, kwaGombe, pamoja na kichanjaani na tatizo tulilifikisha kwa wahusika ambao ni zawa wamesema tatizo ni kuharibika kwa mchikikichi katik kisima kinachosambazia maji katika maeneo hayo na waliahidi wanalifanyia kazi suala hilo lakini ni miezi mitatu sasa inaenda kuwa mwezi wa nne".
Aidha sheha huyo amesema kuwa wamelipeleka suala hili kwa uongozi wa wilaya kwa kupatiwa ufumbuzi zaidi.
Hata hivyo ameiomba serikali pamoja na mamlaka husika kusiaidia kulipatia ufumbuzi suala la kukosekana kwa huduma ya maji katika vijiji hivyo.
Harakati za kumtafuta mkurugenzi wa mamlaka ya maji pemba juu ya suala hili zinaendelea .
Na tutakujuza zaidi.
Mwisho
Comments
Post a Comment