Ahukumiwa kwa kumkashifu Rais
Habari kwa hisani ya Millard Ayo Page
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Simiyu imemuhukumu kifungo cha miaka saba Mtanzania Levinus Kidanabi (Chief Son's) baada ya kutiwa hatiani kwa makosa matatu ikiwemo kumkashifu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan kupitia mitandao ya Kijamii.
Mbali na hilo, pia Kidanabi ametakiwa kulipa faini ya Tsh.Mil 15 ambapo hukumu hiyo imetolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Matha Mahumbuga.
Hakimu huyo amesema kuwa Mtuhumiwa huyo alitoa taarifa ya uongo kinyume cha sheria ya makosa ya kimtandao ya mwaka 2015, ambapo taarifa hiyo aliichapisha kupitia jukwaa la mtandao wa WhatsApp la 'Simiyu Breaking News'
Comments
Post a Comment