DIWANI AONDOA KERO YA VYOO SKULI WALIMU WAFURAHISHWA NA HATUA HIYO ALIYOICHUKUA.

NA AMINA MASSOUD JABIR- PEMBA 

 Hatua zilizochukuliwa na Diwani Mwanamke wa Wadi ya Tibirinzi Chake Chake mkoa wa kusini Pemba kutatua changamoto ya Vyoo pamoja na Barabara kupitia fedha za mfuko wa jimbo katika Skuli ya michakaeni  imewafurahisha wazazi walezi, wanafunzi pamoja na waalimu wa  skuli hiyo    

Wamesema hatua hiyo imesaidia kuboresha zaidi elimu na kupelekea maendeleo bora kwa wanafunzi wa jinsia zote kwani hapo awali mahudhurio yalikuwa tofauti kwa wanafunzi wa kiume na wakike waliofikia baleghe huku wanafunzi wenye ulemavu wakipiatia wakati mgumu.

Wakizungumza na mwandishi wahabari hizi wanafunzi wenye ulemavu wa viungo  Samir Khamis Juma,  Latifa Haji Faki na wenye Ulemavu wa kuona  Amina Juma Omar na Raudhwat Mohammed AbdulRahman wamesema kutengenezwa kwa barabara kunawasaidia kufika Skuli mapema ukilinganisha na hapo awali.
Kwa upande wao wazazi Halima Said Msiuna Hassan Khamis Othman wamesema kutengenezwa kwa Barabara kumepelekea watoto wao kuhudhuria Skuli kwa wakati na kwa upande wawasichana waliofikia baleghe imesaidia kutokukatisha masomo wakiwa katika hedhi 
Kwaupande wake Mwalimu Mkuu Msaidizi Skuli ya Michakaini B Ali Abdalla Makame amesema hapo awali walikuwa na Vyoo sita ambavyo vilikuwa nivibovu nakutumiwa kwa wanafunzi takribani 3,747 kwa Michakaeni Ana B ambapo kwa kila tundu moja lilikuwa likitumiwa na wanafunzi wasiopungua 624 hali ambayo ili kuwa inahatarisha usalama  wa afya zao.
Mwalimu Makame amesema kuwa kwasasa wamejengewa Vyoo 5 na 6 vya awali vimefanyiwa ukarabati ikijumuisha Vyoo 11 na kufikia malengo ya wizara ya elimu kwamba kila tundu moja litumiwe na wanafunzi wa kiume 50 na wakike 45.

Mwalimu wa Michakaini Afatma Haji Ali amesema kupatikana kwa vyoo kumesaidia kumeondoa utoro kwa wanafunzi wa kike wakiwa katika siku za hedhi.

Wanafunzi wa skuli hiyo wamemshukuru diwani huyo kwa kusikia kilio chao na kuwatatulia changamoto hiyo na kusema hatua hiyo itazidi kuboresha elimu ya kuendelea kutoa matokeo mazuri yamitihani ya kitaifa.

Mkubwa Ali Kombo ni naibu sheha wa shehia ya Msingini amesema baada ya kujengwa kwa barabra hiyo kumepelekea maendeleo ya kiuchumi katika kijiji cha michakaini na kupungua kwa vitendo vya kihalifu kwani wanafunzi wengi walikuwa wanakata skuli na kujiingiza katika vikundi viovu.

Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Mohammed Nassor Salim amepongeza jitihada zilizochukuliwa na Diwani huyo kupitia mfuko wa jimbo kwakuwezesha kutatua changamoto hiyo na kueleza kuwa licha ya juhudi hizo zilizofanywa na kiongozi mwanamke lakini pia Serikali kupitia Wizara hiyo inalengo la kujenga Vyoo 781 na kutengeneza Taula za kike Skuli zote za Pemba lengoni kuboresha elimu na kuwaweka wanafunzi katika mazingira salama.

Kwa upande wake Diwani wa Wadi yaTibirinzi Fatma Juma Khamis amesema aliamuakulivalia njunga suala la utengenezaji wa Vyoo na Barabara vya skuli hiyo kufuatia shida wanazozipata wanafunzi pamoja na wanajamii wanaotumia Barabara hiyo hususani watu wenye Ulemavu.
Jumla ya shilingi milioni 24zimetumika katika ujenzi wa vyoo 5 na ukarabati wa vyoo 6 ndani ya skuli Michakaeni A na B, na shilingi milioni 1 zimetumika katika kukarabati Barabara kwa hatua ya kifusi. 

MWISHO

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI