POLISI ZANZIBAR IMEWAKAMATA WATU 6 KWA TUHUMA ZA WIZI NA UNYANG'ANYI KWA WATALII NA WENGINE 29 KWA MAKOSA MBALI MBALI



NA OMAR HASSAN NA SAID BAKAR - UNGUJA .        

Jeshi Polisi Kamisheni ya Zanzibar linawashikilia watumiwa sita kwa wizi na unyang'anyi wa kutumia silaha za jaji dhidi ya watalii na wengine 29 kwa Makosa  mbali mbali.

Hayo yamebainishwa na Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad huko kizimkazi Mkoa wa Kusini Unguja alipokua akisikiliza kero na changamoto za uhalifu za wananchi wa Kijiji hicho.

Amesema watuhumiwa hao wamekamatwa kufuatia msako maalumu dhidi ya wahalifu katika maeneo ya kitalii unaoendelea kufanya na Jeshi hilo.

Watuhumiwa waliokamatwa ambao wanatuhumiwa kuhusika katika matukio matatu ya kuwaibia wageni na kupatikana na baadhi ya vitu vya wageni ni pamoja na Hamidu Abdalla Hassan miaka 22 mkaazi wa Kibanda maiti, Mtumwa Jumanne Mtumwa miaka 32 wa Nyarugusu na Said Khalfan Said miaka 25  mkaazi wa Kizingo.

Wengine ni Khelef Ali Khelef miaka 30 mkaazi Mwera, Mikidadi Ramadhan Idi miaka 45 mkaazi wa Sebleni na Juma Ajuwedi Juma miaka 36 mkaazi wa Bwejuu.

Kamishna Hamad amewataka wananchi kuwafichua wahalifu na kuwatambua wageni wanaoingia katika vijiji vyao kuzuwia uhalifu na kuweka mazingira salama kwa watalii wanaoingia nchini.

Katika hatua nyengine Kamishna Hamad amewasihi wananchi wa Kizimkazi kukaa pamoja na ndugu zao wa Muyuni kutatua mgogoro wa ardhi uliopo baina ya vijiji hivyo. 

Mapema Wananchi wa Kizimkazi wameiomba Serikali kuingili kati na kuutatua mgogoro huo kabla ya kusababisha madhara.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI