MASHIRIKIANO KUDHIBITI MAAFA KWA WATOTO YANAHITAJIKA.
NA FATMA SULEIMAN - PEMBA
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Mh. Leila Muhammad Mussa amewataka watendaji wa serekali kufanya kazi kwa mashirikiano Ili kuwaepusha wanafunzi na maafa na kuwaacha wakiwa katika mazingira salama ya kutafuta elimu.
Waziri Lela ameyasema hayo Leo katika ziara yake ya siku moja katika Skuli ya uwandani msingi mara baada ya kutokea tatizo llililoshukiwa Kua lilitokana na wanafunzi kuchezea kemikali ambazo zimeshamaliza Muda wake wa matumizi.
Amesema ni wajibu wa Kila mtendaji kusimamia ipasavyo majukumu yake katika kuhakikisha wanaweka mazingira mazuri na ya usalama kwa wanafunzi na kuacha kuwaeka wanajamii katika taharuki .
Katika hatua nyengin waziri ameitaka ofisi ya Mkemia Mkuu kuondoa kemikali ambazo zimeshapitwa na wakati Ili kuwaeka wanafunzi katika mazingira salama na kuepusha taharuki kwa wanafunzi hao na jamii kwaujumla.
Kwa Upangde wake Mkuu wa Mkoa wa Kusini Pemba Mh. Matar Zahor Masoud Amewapongeza watendaji wa serekali kwa juhudi ambazo zimechukuliwa za kuwasaidia wanafunzi hao ambao walipatwa na tatizo kutokana na kushika kemikali hizo.
Aidha Mh. Matter amemtaka Mkemia kuchukua hatua za mara Moja katika kuhakikisha kwamba wanafunzi wanasoma katika mazingira salama.
Nae Daktari dhamana wa hospital ya Chake Chake Dkt. Sharifu Hamad Khatibu amesema mara baada ya wanafuzi hao kufika katika hospital aliamua kuwapatia huduma huku akiendelea kuchunguza ni aina gani ya ugonjwa ambao uliwapata wanafunzi hao.
Nae Kaimu Mratibu wa Maabara ya Serekali Pemba Seif Ali Hamad amesema mara baada ya kutokea tatizo Hilo wameamua kuchukua hatua za haraka huku wakiendelea kuchunguza Ili kujua ni kemikali ya aina Gani ambayo imechezewa na wanafunzi hao .
Kwa upande wa Walimu Wakuu wa skuli ya Uwandani Msingi Halima Saidi Ali na Mwalim wa Skuli ya Sekondari Uwandani Hamis Ali Abdalah wamesema kuwa mara baada ya kutokea tatizo Hilo waliamua kuwataka wanafunzi kunawa mikono kwani awali hawakujua kua wanafunzi hao walichezea kemikali .
Comments
Post a Comment