WAANDISHI WAFUNDISHWA MBINU ZA KUJIKINGA NA UHALIFU WA MITANDAONI
- Get link
- X
- Other Apps
NA A-MINA AHMED MOH’D - PEMBA
Waandishi wa Habari Kisiwani Pemba wameaswa kuzidisha umakini katika utumiaji wa mitandao ya kijamii ikiwa ni pamoja na kuweka ulinzi katika utumaji wa taarifa zao ili zisiweze kudukuliwa.
Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Clabu ya waandishi wa Habari ksiwani Pemba Pemba Press Club Bakar Mussa Juma Alipokuwa akifungua mafunzo ya Siku moja ya Usalama Wa Mitandao (Digital Security) kwa waandishi wa habari wanaotumia zaidi mitandao ya kijamii katika kazi zao yaliofanyika katika ukumbi wa ofisi hizo Misufini Chake Chake.
Alisema mitandao imekuwa ikipeleka ujumbe kwa haraka zaidi kwa jamii ukilinganisha na vyombo vyengine vya habari vilivyopo na kupelekea kutikuwepo kwa usalama kwa waandishi wa habari kutokana na baadhi ya wahalifu kutumia mitandao hiyo kwa kudukua taarifa pamoja kufanya uhalifu .
"Kudukuliwa taarifa kwa mitandao ya kijamii aidha za mwandishi mwenyewe lakini hata kazi za kihabari zinazofanywa na kutumwa katika mitandao , Pia unaweza kupata taarifa nyingi na ukazitumia katika vyombo vyako vya habari lakini changamoto ikaja kuwa habari nyengine ni za uongo kwa vile hujazifanyia uchunguzi wa kina na kuwa chanzo cha matatizo".
Aidha Amewataka waandishi Hao kuyafanyia kazi mafunzo watakayopatiwa juu ya suala hilo la usalama wa mitandao ili kuweza kujiweka salama katika utumiaji wao.
"Kujiepusha na mitandao ambayo haiko Salama kujiepusha kutofautisha fake news, kutasaidia kuwaepusha kujiingiza kwenye mashaka , kuweza kulinda taarifa zako tuyafanyie kazi mafunz haya tutakayo patiwa leo ambayo lengo lake ni kusaidia kujua kuilinda na kuitumia bila wasi wasi kwenu.Alisema.
Kwa Upande wake Mratibu wa Club hiyo Mgeni Kombo Khamis aliwataka washiriki wa mafunzo hayo kufikisha elimu watakayopatiwa kwa waandiahi wengine ambao wamekosa fursa hiyo kutokana na sababu mbali mbali.
Akitoa Elimu ya Usalama wa mtandao kwa waandishi hao mkufunzi Aliepatiwa Mafunzo hayo na Umoja wa Club za Waandishi wa Habari Tanzania UTPC Haji Nassor Muhamed pamoja na mambo mengine alisema kuwa usalama wa mtandao ni kujikinga na hatari zinazoweza kujitokeza kwa watumiaji wa mtandao katika kujikinga na hatari zilizokusudiwa na wahalifu na zisizokusudiwa.
HAJI NASSOR MUHAMED - MKUFUZI MAFUNZO DIGITAL SECURITY.
"kuna uhalifu katika mitandao ambao umepangwa na ule uliokuwa haukupangwa yapo mavitu mbali mbali usiyahitaji unaweza ukayakuta katika simu au komputa yako , masuala ya kufungilua email ya mtu kumuazima mtu mwengine, afungue, yote ni hatari ili ujikinge ni lazima ujue Usalama na ulinzi"Alisema.
Waandishi hao walifundishwa mambo mbali ya usalama wa mitandao ikiwa ni pamoja na Kujikinga dhidi ya hatari (Safety) kujikinga binafsi ili kuweza kuwa salama katika matumizi ya mitandao kwa vyombo vya mitandao (Security) Tathmini ya hali ya hatari pamoja na mbinu za kujua program hatarishi na zisizo hatarishi ambapo katika mafunzo hayo pia waandishi hao wameaswa kujiunga na club ya waandishi wa habari ili kuweza kupata fursa mbali mbali.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment