Tumieni Maji kwa uangalifu
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amewataka Wananchi wa Dar es Salaam na maeneo ya jirani kuwa na matumizi mazuri ya maji wakati huu wa kiangazi kwa kuwa kina cha maji kwenye chanzo cha Mto Ruvu kimepungua kwa asilimia kubwa.
Makalla akiwa kwenye ziara ya kutembelea chanzo cha maji cha Ruvu juu na chini amesema upungufu wa maji kwenye chanzo cha maji cha Mto Ruvu umesababishwa na ukosefu wa mvua za vuli na uwepo wa kipindi kirefu cha kiangazi.
"Sote tulitarajia kuwepo kwa mvua za vuli kwa kipindi hiki ambazo zingesaidia kuongeza kiasi cha maji kwenye Mto Ruvu na kuwezesha upatikanaji wa maji kwa Wananchi”
"Lakini kulingana na utabiri wa Mamlaka ya hali ya hewa ambao ulieleza kuwa kutakuwa na kipindi kirefu cha kiangazi, imesababisha kupungua kwa maji, hivyo kutakwepo na mgao wa maji kwenye maeneo ya mijini”
"Uzalishaji wa maji kwenye chanzo cha Mto Ruvu ni lita milioni 466 kwa siku lakini kwa sasa uzalishaji umepungua mpaka lita milioni 300 sawa na asilimia 64”
#MillardAyoUPDATES
Comments
Post a Comment