EPUKANANENI NA MIGOGORO.

NA OMAR HASSAN-   UNGUJA 

JAMII IMETAKIWA KUFUATA TARATIBU ZA MANUNUZI YA ARDHI ILI KUEPUSHA MIGOGORO YA ARDHI INAYOSABABISHWA NA MATAPELI WANAUZA ARHI ZA WATU KWA NJIA YA UDANGANYIFU.

WITO HUO UMETOLEWA NA KAMISHNA WA POLISI ZANZIBAR HAMAD KHAMIS HAMAD ALIPOKUA AKIZUNGUMZA NA WANANCHI WA SHEHIA ZA MWANYANYA, SHARIFUMSA, KIBWENI NA MTONI HUKO UWANJA WA SKULI YA SHARIFUMSA MKOA WA MJINI MAGHARIBI ALIPOKUA AKISIKILIZA KERO ZA UHALIFU KATIKA SHEHIA HIZO.

 AMESEMA KUMEKUA NA MATUKIO MENGI YA UTAPELI WA ARDHI KWA BAADHI YA WATU KUUZA ENEO MOJA LA ARDHI KWA WATU ZAIDI YA MMOJA NA BAADHI YA WATU KUUZA ARDHI AMBAZO SIO ZA KWAO KUNAKOSABABISHWA NA KUTOFUATA TARATIBU ZA MANUNUZI.

KATIKA HATUA NYENGINE KAMISHNA HAMAD AMEWATAKA WANANCHI KUTOSHAWISHI KUTOA RUSHWA KWA ASKARI WA JESHI LA POLISI KWANI KUFANYA HIVYO NI KUCHOCHEA VITENDO VYA RUSHWA AMBAVYO VINAZUIA UWAJIBIKAJI NA HUKOSESHA HAKI ZA WANANCHI.

AIDHA AMEELEZA KUWA ATAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA ASKARI WA JESHI LA POLISI WATAKAOJIHUSISHA NA VIOTENDO VYA RUSHWA HIVYO AMEWAOMBA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA ASKARI WANAOJIHUSISHA NA RUSHWA ILI WACHUKULIWE HATUA ZA KISHERIA.

KWA UPANDE WAO WANANCHI WAMELIPONGEZA JESHI LA POLISI KWA KUWAPELEKA WAKAGUZI WA POLISI KATIKA KILA SHEHIA AMBAO WANASHIRIKIANA  KATIKA KUKABILIANA NA UHALIFU.

MWISHO 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI