ZAWA YA WATAKA WANANCHI WALIOLALAMIKA KUKOSA HUDUMA HIYO KUVUTA SUBRA TATIZO LINASHUGHULIKIWA.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA
Mamlaka ya maji Zanzibar zawa kisiwani pemba imesema inendelea na zoezi la usafirishaji wa mabomba makontena na pampu kutoka kisiwani unguja ili kupeleka na kuendeleza harakati za uboreshaji na ubdilishaji wa mabomba na mashine katika baadhi ya maeneo ambayo yanayokosa pamoja na kupata kwa mgao huduma ya maji .
Mamlaka hiyo imewataka wananchi kisiwani humo kuendelea kusatahimili kutokana na kukosa huduma ya maji safi na salama katika meneo yao ambapo imesema mamlaka hiyo inaendelea kulipatia ufumbuzi suala hilo ili waweze kupata huduma hiyo bila ya usumbufu kama ilivyokuwa awali.
Akizungumza na habari hizi kwa niaba ya mkurugenzi wa mamalka hiyo kisiwani pemba Ofisa Mahusiano mamlaka ya maji zawa Sleiman Anass Massoud amesema mamlaka inaendelea kufuatilia upatikanaji wa mashine itakayosaidia kufikisha maji katika vijiji hivyo jambo ambalo tayari limefanikiwa kwa hatua kubwa hadi kufikia sasa.
"Tunaendelea na utaratibu tu wa usafirishaji wa vifaa ili kuweza kurejesha huduma ya maji pamoja na mashine zilizounguwa kufungwa mpya
katika baadhi ya visima vilivyoungua mashine"
"Lakini pia tunaendelea kutekeleza miradi ambayo itakapomalizika itakwenda kumaliza kabisa tatizo la maji kisiwani pemba kwa maeneo yote".
" Ni kweli Tatizo lipo katika vijiji hivyo na sababu ni mashine iliyopo katika kisima kilichopo chambani kwa popo ambayo ndicho kinachopeleka maji katika maeneo ya kwa gombe kichanjaani pamoja na maeneo jirani imeharibika lakini mamlka inaendelea kulipigia mbio kulipatia ufumbuzi suala hili "
Amesema Tayari mashine zipo bandarini katika makontena ambapo mara zitakapofika kisiwani pemba moja kati ya mashine hizo itatumika katika kisima hicho.
Aliongeza kuwa" Kuthibitisha kwamba suala la kukosa huduma ya maji wananchi wetu sisi mamlaka linatukosesha raha tumemuomba Makamo wa pili wa rais kutusaidia kufunguliwa kwa urahisi makontena ambayo yana vifaa vya maji vilivyotoka oman ambayo yapo bandarini vifanyiwe urahisi vitolewe na viweze kugawiwa vitakavyoletwa pemba viletwe na vitakavyobaki unguja vibakie
"Na mkurugenzi wetu hivi ambavyo tunaongea yupo unguja anashuhulikia suala hilo ili wananchi wasiendelee kuteseka maji ndio uhai Alisema".
" Aliongeza kuwa Mashine iliharibika na kuungua tulitengeza kuona kama itakubali tuweze kuirudisha lakini haikukubali tena hivyo zipo mashine ambazo zimeagizwa na mda wowote kutoka sasa zitafika kisiwani pemba kwajili ya visima mbali mbali moja kati ya visima hivyo ni kisima cha popo kilichopo Chamabani" .
Aidha alisema kuwa Mamlka haikuwa na namna nyengine juu ya suala hilo kutokana na mashine iliyoharibika kutokubali kupandisha maji kupeleka katika vijiji hivyo licha ya matengenzo iliyofanyiwa.
"Mashine iliharibika mia fil mia ililazimika ipatikane kama ile iliyoungua ambayo ni 11kilowat tu kusafirishia maji tulijarivu kuingiza mashine kubwa haikukubali tukaitoa ndio mana tatizo likadumu kwa muda wa miezi sasa kwa vile ililazimika kupatikana mashine (Pampu) kma ile tunasubiri kuipokea tu kisiwani pemba kuweza kuwatatulia shida hiyo.
Alisema ni kweli maji ndio kitu muhimu katika harakati za kila siku ambapo amewaahidi wanachi hao kutegemea mambo mazuri kutoka mamlka ya maji ambapo amesema lich hatua hizo lakini pia katika maeneo yao ujenzi wa tangi kubwa la maji unaendelea ambapo utakapokamilika utasaidia juwaondoshea shida ya maji wananchi wote.
Aidha Afisa huyo ametaja baadhi ya meneo ambayo mamlka inaendelea kuyasimamia kupata ufumbuzi kumaliza tatizo la kukosa hudua ya maji safi na salama kutokana na kupata maji kwa mgao huku mengine y kikosa kabisa kisiwani pemba katika wilaya ya chake chake wete micheweni na mkoani
ambapo ameyataja maeneo hayo kuwa ni pamoja na kichanjaani, Chanjani, kwa Gombe, Pujini dodo, Kilimni banaani madungu chanjaani, Chuchuu, Shaurikani, Mjana pweza, Matale, kitwea, Mtangani Mtambile Chambani, pandani, Makangale, Kiuyu maziwa ngombe pamoja na kiuyu mjini
Katika hatua nyengine Afisa huyo amesema kuwa mamlaka hiyo inaendelea na ujenzi na uchimbaji na uboreshaji wa visima vya maji pamoja ma ujenzi wa matangi ili kuendelea kuwapatia huduma bora zaidi wananchi maeneo ya miji vijiji.
"Tunaendelea kubadilisha mabomba kuchimba visima pamoja na kulaza mabomba mapya takriban maeneo yote ya wilaya kisiwani pemba na hii ninkutokana na kuongezeka kwa matumizi ya maji yatakayisaidia kuondoa usumbufu maeneo hayo nikiyoyataja na maeneo mengine.
"Yapo mabomba ambayo kutokana na kuongezeka mahitaji kwa sasa yamekuwa hayatoshelezi, mengine ni bomba chakavu jambo ambalo linasababisha baadhi ya vijiji hivyo kupata maji kwa mgao. "
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment