TUSHIRIKIANE KUTOA TAARIFA ZA UHALIFU.
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA
Mkuu wa wilaya Ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali amewataka wananchi wa wilaya hiyo kuendelea kutoa mashirikiano katika kudhibiti vitendo vya uhalifu kwa kutoa taarifa kwa vyombo vya sheria husuan ni katika meneo yenye bandari zisizo rasmi katika wilaya hiyo.
Amesema Mashirikiano wanayoendelea kuyatoa kwa serikali na jeshi la Polisi kuripoti taarifa za kiuhalifu zinazijitokeza imekuwa chachu ya kudhibiti mali za serikali zisiuzwe kinyemela ikiwemo Makonyo na karafuu.
"Wananchi wa kaazi chake chake suala la kupambana na vitendo vya kihalifu ni suala la kila mmoja wetu sio la serikali peke yake mashirikiano mnayoonesha kupambana na masuala haya ni vyema tuyaendeleze kutoa taarifa serikali iweze kuchukua hatua."
Aidha aliwataka wananchi wanaokaa katika maeneo ya bahari kutoa taarifa za uingiaji wa wageni katika maeneo yao ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria.
" wapo baadhi ya watu hutumia maeneo ya bandari zisizo rasmi kuingiza na kusfirisha bidhaa lakini pia wageni kutoka meneo mengine wananchi msisite kutoa taarifa kama hizi zitasaidia kuimarisha usalama" .
Alisema Mashirikiano hayo yanaendelea kuzaa matunda katika kudhibiti upotevu wa mali za serikali ambazo bila kudhibitiwa na wananchi kutoa taarifa zingefanikiwa kupoyea na kupoteza pato la taifa.
" Ni juzi tu tumewakamata baadhi ya wananchi wasiopemdabkufuata sheria wakiwa na polo zaidi ya 80 za makonyo Makavu wakiwa tayari wanayasafirisha kupitia bandari zisizo rasmi lakini wananchi walitoa taarifa askari wetu wa kmkm pamoja na uongozi wa wilaya ulifika na kunusuru ".
Katika Hatua nyengine Mkuu wa wilaya hiyo Amewapongeza wananchi wa wilaya hiyo kwa kuendelea kutumia Shirika la biashara la ZSTC kuuza karafuu zao kwa mujibu wa sheria.
" Niwatake wananchi waendeleze suala hili la uuzaji wa karafuu zao katika maeneo yaliwekwa na serikali pia niwapongeze kuona wananchi wanayatumia vyema hadi sasa hakuna taarifa za kuwepo kwa waliokiuka agizo hilo nankuuza kimagendo.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment