KIONGOZI MWANAMKE ANAEONGEZA KASI YA MAENDELEO KATIKA MKOA WAKE NDANI YA KIPINDI KIFUPI CHA UONGOZI. Uboreshaji wa huduma Muhimu za kijamii ikiwemo Maji, Skuli, Masoko Na vituo vya Afya. Usimamiz bora uwajibikaji i na utayari wa utendaji kazi waelezwa kuchagia kasi hiyo

NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA NI KIPINDI Cha Miaka Miwili ( 2) Tangia Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi Kumteua Salama Mbarouk khatib Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Kushika Nafasi hiyo ambapo Mnamo Siku yaTarehe 1/12/2020 Alimteua Rasmi kushika nafasi hiyo. Ni Salama Mbarouk khatib ni Mwanamke 1 Pekee alieteuliwa katika Serikali ya Awamu ya nane ya Mapinduzi ya Zanzibar kati ya Wakuu wa Mikoa 5 waliopo Zanzibar ambapo ni sawa na asilimia 20 ya viongozi wote ambao wameshika nafasi hiyo kwa wanawake . Zanzibar ina jumla ya Mikoa 5 Mitatu kati ya hiyo inapatikana kisiwani Unguja na Miwili iliyosalia ikiwa ipo kisiwani Pemba. Mabadiliko makubwa yanaendelea kujitokeza katika Mkoa Wa Kaskazini Pemba katika kipindi Kifupi cha Miaka Miwili. Miingoni Mwa Mabadiliko hayo ni pamoja na Ujenzi wa Matangi ya kuhifadhia Maji, Vituo vya Afya, Skuli, Umem...