DC CHAKE ATOA NENO KWA WATENDAJI WA ZRB.
Na Amina Ahmed Moh’d - PEMBA
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Abdalla Rashid Ali amesema uhusiano nzuri baina ya Bodi ya Mapato Zanzibar(ZRB) na Wafanyabiashara utatanua wigo katika kuongeza katika ukusanyaji wa Mapato.
Mkuu wa Wilaya huyo ameyasema hayo leo huko Katika ukumbi wa ZRB Gombani alipokuwa. akizungumza na Wafanyabiashara wa kisiwani Pemba ikiwa ni katika wiki ya kurejesha shukurani na furaha kwa mlipa kodi.
Amesema wao kama viongozi wanajukumu ya kusimamia mipango ya serikali watatumia nafasi zao kuwaunganisha wafanyabiashara na ZRB ili kila mmoja aweze kutekekeza majukumu yake kwa ufanisi bila ya kuwepo kwa mivutano.
Mapema Mkurugenzi wa ZRB Pemba Jamal Hassan Jamal amewataka wafanyabiashara kuondelea kulipa kodi kwa hiari.
Wakizungumza kwenye mkutano huo baadhi ya wafanyabiashara wa kisiwani Pemba wameendelea kuomba kuondoshewa changamoto zilizopo ikiwemo kodi kubwa ambazo ni kikwazo kwa maendeleo yao
Pamoja na michango uliotolewa na Wafanyabiashara hao wameomba kukutanishwa na Kamishna wa ZRB na uongozi wa Wizara ili kuwasilisha kwao malalamiko waliyo.
Comments
Post a Comment