Viongozi wa chama waaswa na Jeshi la Polisi.
- Get link
- X
- Other Apps
Na Amina Ahmed Moh'd.
JESHI la polisi Mkoa wa kusini Pemba limewashikilia na kuwahoji watu wawili kwa tuhuma za kutoa maneno ya uchochezi na matusi dhidi ya viongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar juu ya kupinga uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar Ndugu Thabit Idarous faina na kusambaza kashfa na maneno hayo katika mitandao ya kijamii .
Watu hao ambao ni Salum Abdalla Herezi (maarufu Mwalim Herezi ) ( 65 ) ambae ni mjumbe wa kamati ya uongozi jimbo la Mtambile Kupitia chama cha ACT wazalendo mkaazi wa Mjimbini wilaya ya Mkoani pamoja Nachia Ali Jamali ( 39) mjumbe wa kamaati ya fedha jiombo la Chamabani kupitia chama hicho mkaazi wa wambaa Mkoa wa Kusini Pemba.
Akitoa Taarifa kwa waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa kusini Pemba ACP Abdalla Hussein Mussa alisema watu hao ambao ni wafuasi wa chama cha ACT wazalendo wameshikiliwa siku ya tarehe 10 kwa nyakati tofauti kufuatia doria maalum iliyofanywa na jeshi hilo katika maeneo mbali mbali ya Mkoa huo ikiwa ni harakati maalum za kuendelea kuimarisha ulinzi na usalama katika maeneo tofauti ndani ya Mkoa huo.
ABDALLA HUSSEIN MUSSA -ACP KUSINI PEMBA.
Alisema kuwa mnamo siku ya tarehe 5/12 / 2022 majira ya saa nne mpka saa sita za mchana katika ofisi za chama cha ACT wazalendo eneo la Mtambile Mkoa wa kusini Pemba wakiwa katika kikao cha ndani ya chama hicho viongozi hao walitoa maneno ya kashfa na matusi dhidi ya viongozi wa chama cha Mapinduzi na kusambaza katika mitandao ya kijamii Jambo ambalo ni kosa.
Aidha jeshi hilo limesema bado linaendelea na upelelezi juu ya suala hili na mara jeshi litakapokamilisha upelelezi huo litakapofanikisha upelelezi huo hatua nyengine za kisheria zitachukuliwa ikiwemo kufikishwa mahakamani wale wote watakaotiwa hatiani Juu ya uchochezi pamoja na usambazaji wa kashfa hizo katika mitandao ya kijamii.
Aidha Jeshi La polisi Mkoa wa kusini Pemba limewataka Viongozi wa vyama vya siasa Kutumia vyema uhuru na fursa iliyotolewa kufanya mikutano ya ndani kwa kuzinagatia sheria kanuni na taratibu ya ufanyaji wa mikutano hiyo.
Katika hatua nyengine kamanda huyo Alisema kuwa hali ya ulinzi na usalama katika Mkoa huo inendelea vyema kutokana na mashirikiano yanaoendelea kutolewa na wananchi .
MWISHO
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment