LICHA YA JUHUDI KUCHUKULIWA NA VIONGOZI WA SHEHIA GOMBANI BADO WALIA KUKOSA HUDUMA YA MAJI MIEZI SABA SASA .
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D
UKOSEFU wa huduma ya maji katika Baadhi ya Maeneo Shehia ya Gombani wilaya Ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Waathirika wakubwa ni wanawake na watoto.
Harakati hizi Mapema leo Asubuhi zilifika ili kuthibitisha kilio hicho na kamera za Habari hizi zikawaanasa Baadhi ya watoto wakitembea masafa marefu huku wakiwa na ndoo kichwani wakitoka kuifata huduma hiyo Katika eneo la Msikiti Uliopo karibu na Ofisi za Serikali Huku wengine wakionekana kuelekea huko kuifata huduma hiyo.
Sheha wa Shehia ya Gombani Subira Abdalla Juma akizungumza na habari hizi Alisema kuwa Upatikanaji wa huduma ya Maji katika shehia hiyo umekuwa mkubwa licha ya ya Uongozi wake kuchukua hatua mbali mbali.
"Tatizo hili la ukosefu wa Maji Safi na Salama Gombani si baadhi ya Maeneo tu nasubutu kusema ni Gombani nzima hapo mwanzo yalikuwa yanapatikana walau baadhi ya maeneo lakini saivi ni mote inakaribia Miezo saba kama sio Mwaka.
" Napiga kelele kulisemea tatizo kadri ya uwezo wangu kwa Viongozi wa juu, Mpka Serikali ya wilaya inatusaidia ilitoa ruhusa kuzibuliwa kwa Tangi Lililopo nyuma hospitali ya Chake Chake ili tupate Maji yalikuja siku mbili hayakuja tena" .
"Wawakilishi wetu na wabunge Tuliwatafuta tukawaelezea suala hili walipofuatilia Zawa waliambiwa ni Transoma wakajitolea ikaletwaimefungwa siku mbili halo ikawa ni ile ile tukaenda kuwalilia tena wakaambiwa Mchikichi wametuletea lakini kiukweli nao haukusaidia mana tuliambiwa umeharibika hatujajua bado tatizo ni nini Gombani mana Tumeshajitahidi na visima vipo vingi lakini maji hatupati.
Aidha Subira Alisema kuwa usumbufu huo wa kukosa huduma ya Maji kijiji kizima cha Gombani ni takribani Mwezi wa Saba Sasa ambapo wananchi wake hulazimika kutafuta maji kwa majirani ambao wamechimba visima katika majumba yao Huku wengine kusubiri Lulu hiyo katika baadhi ya miferji ambayo yanatoa maji kwa baadhi ya wakati.
" Siku moja moja kuna baadhi ya nyumba mifereji yao hutoa maji apo tena watu hupigiana simu wakaenda kupanga foleni watu hawamalizi yanakatwa ,,Wengine wanapata maji kwa majirani ambao wamechimba visima ndani mwao tena hiyo usiku, siku nyengine asubuhi, leo nyumba hii kesho ile binafsi mimi mwenyewe namaliza mitaa kufuata maji apa kidutani kuna nyumba moja tu inayotoka maji.
Alieleza kuwa Shehia ya Gombani yenye wakaazi 4835 ambao wao ni wanawake na watoto wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli zao kwa wakati kutokana na usumbufu huo .
Wakizungumza baadhi ya wakaazi wa kijiji cha Madina Shehia ya Gombani wameiomba serikali kutolifumbia macho tena suala hili na badala yake kuwatafutia njia ya kulimaliza Tatizo hili ambalo limeuwa kikwazo ha maendeleo.
"Gombani ni shehia amayo ipo mjini kabisa vijijini hakuna shida ya maji ajabu ipo hapa tu leo maji yanatoka kesho hayatoki inatuumiza sana hii, Watoto hawana muda na kucheza lazima watusaidie kuyatafuta maji hatuna namna akina baba hawasubutu kutafuta kijio na Kuoanga foleni mzigo unatuelemea. Alisema Bi Rahma .
Akizungumzia Suala hili Ofisa Uhusiano kutoka Mamlaka ya Maji Zanzibar zawa Ofisi ya Pemba Suleiman Anass Massoud Alisema kuwa Mamlaka hiyo inaendelea kulipatia ufumbuzi tatizo la ukosefu wa Maji Shehiaya Gombani na baadhi ya shehia jirani ili kuondoa shida kwa wananchi.
" Nikiri kuwa mara kwa mara tumekuwa tukipokea taarifa kutoka Shehia ya Gombani wakilalamikia ukosefu wa huduma ya maji Safi na Salama nikiri hilo, Viongozi wao wanatupigia mara kwa mara simu, Sio mara moja wala mara mbili ni kipindi sasa lakini naomba tufahamu kuwa Sio Gombani yote kama inakosa maji, ni baadhi ya maeneo na Structure ya Gombani wanapata maji kwa vianzio tifauti yapo maeneo wanayopata maji kupitia Tangi la Machomane ambayo ni ya mgao , kuna baadhi wanapata kupitia kisima cha Ng'ambwa na wegine wanapata Kupitia kisima cha Gomban Mchuwa,kwamana iyo utakuta inamapande mapande utokaji wake wa maji.
Aidha Ofisa huyo alisema kuwa Tathmini ya jumla ya upatikanaji wa maji katika Shehia hiyo linaukubwa ambapo alisema kuwa baadhi ya maeno yamekuwa hayafikiwi kwa sasa ni pamoja na Gombani Madina, Mchuwa, Gombani ya kati, Uwanja Mkongwe.
Hata hivyo Ofisa guto Alisema kuwa Mamlaka inaendelea na mipango miwili mikubwa ya kumaliza tatizo la ukosefu wa maji Gombani.
"Kwanaz tumejaribu kubadilisha mtandao wa maji kutoka katikatangi la maji Gombani ambalo linapokea maji kutoka maeneo ya Ndagoni na wesha tumeunga bomba la nchi 4 Kusaidia Baadhi ya Sehemu ambapo kazi hii inasiku ya nne saivi, na tunatarajia kupata mrejesho kamili jumatatu kuona imefikia wapi lengo kuweza kuona Mpango huo unasaidia kupatikana maji maeneo ya Gomban Madina ambayo imekuwa haipati na baadhi ya sehemu nyengine.
Aliendelea kuwa " Uhakika mkubwa ambao upo kwa Wakazi wa Gombani ni kuwa mamalka imekamilisha uchimbaji wa visima3 kati ya visima 5 ambavyo vilikuwa vinahitajika, Bomba kubwa ambalo limepimwa kutoka maeneo ya Ng'mbwa Mpka kufika eneo la Gombani Getini, na bomba hilo litapokea maji kutoka katika visima hivyo vitatu vipya ambavyo tumevichimba juzi, tayari vimeshakamilika, Tunachosubiri ni kupigwa mtaro, na hii kampuni ambayo tumikabidhi kazi, tunamaliza taratibu hizi za utowaji wa tenda, kama miongozo ya Serikali inavyoelekeza zimejitokeza nyingi zimeomba kwaio tayark moja tumeshaona kuwa na muelekeo wa kupata tenda hiyo.
Alisema kuwa baada ya kuanza kuchimbwa mitaro hiyo bomba hiyo itaanza kutoa huduma ya maji katika maeneo ya Mkoroshoni, Mkanjuni na Gombani na Kwale kuondoa kwa asilimia kubwa tatizo la Maji.
Aidha Suleiman aliwataka wananchi Wa Gombani kuvuta subira na uenelea kupata maji hayo kwa Mgao na kuahidi kuwa Changamoto hiyo italata uhakika wa kumalizika mwanzoni mwa January 2023.,Huku miradi mikubwa ya Maji ikiwemo Ujenzi wa matangi na Visima inatarajiwa kuondoa tatizo la Ukosefu wa Maji Pemba kumalizika Katika kipindi cha February Machi baada ya kukamilika kwa miradi mbali mbali inayoendelea kujengwa kwa Fedha za ahueni ya uviko 19 Kusini na Kaskazini.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment