WAFANYA BIASHARA WAFURAHISHWA NA MASHIRIKIANO WANAYOYAPATA KUTOKA BODI YA MAPATO ZANZIBAR ZRB.
- Get link
- X
- Other Apps
Na AMINA AHMED MOH’D
WAFANYA biashara wa bidhaa mbali mbali Katika Mji Konde Mkoa wa Kaskazini Pemba wameishukuru Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB kwa kuendelea kuwapa elimu Mashirikiano pamoja na maelekezo mbali mbali ya ulipaji wa kodi kwa njia sahihi .
Wametoa Shukurani hizo walipokuwa wakizungumza mara baada ya kutembelewa na kupewa Elimu na Ofisa kutoka bodi hiyo ikiwa ni shamra shamra za wiki ya Mlipa kodi
Wamesema Masirikiano hayo wanayoyapata kutoka kwa bodi hiyo yanasaidia kupata ufumbuzi wa changamoto mbali mbali zonazohusu ulipaji wa kodi pamoja na utumiaji wa mashine na utowaji wa Risiti za Kielectroniki .
"Tunapata mashirikiano katika kutatua changamoto mbali mbali zinazohusu biashara zatu lakini ulipaji wa kodi tunapata Elimu inayosaidia katika masuala ya biashara., Awali tulikuwa tunawakimbia tukisikia wanakuja tu tulikuwa tunaona kama ni usumbufuni kwa sababu Hatukuwa na uelewa lakini mashirikiano yao leo hii tunajifunza mambo mbali mbali mfano mashine Alisema Abdi Abdalla Omar Mfanya Biashara Konde.
Hata hivyo wafanya biashara hao wameiomba bodi hiyo kuwasaidia kuwatatulia baadhi ya changamoto ambazo zimekuwa zikirudisha nyuma harakati zao
Tunaomba mtusaidie kupunguza changamoto ya usafirishaji wa mizigo lakini tunaomba mtuwekee usawa kwa ulipaji kodi kuwe na asilimia sawa isiwe wengine wanapata ndogo wengine kubwa kwa bidhaa moja, Alisema Muhammad Gharib Moh’d.
Akizungumza Mkurugenzi wa Bodi hiyo pemba Jamal Hassan Jamali Alisema Bodi hiyo itaendelea kutoa elimu kwa wafanya biashara ili kuzidisha uelewa juu ya Ulipaji kodi pamoja na kuzipatia ufumbuzi baadhi ya Changamoto zilizotolewa na wafanya biashara ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji uelewa zaidi ili kuacha kuona kama ni changamoto.
"Tupo Hapa Micheweni leo Katika Mji huu wa konde ikiwa ni Wiki ya Mlipa kodi Maofisa wetu kwa pamoja tunatoa elimu kwa wafanya biashara lakini pia tunabadilishana mawazo na walipa kodi wet, wamefurahi kwa ujio huu lakini pia wametupa changamoto zao na sisi tumezichukua kuona vipi tunabadilisha uelewa kwa kile ambacho wamehisi kwao ni Changamoto Alisema Mkurugenzi.
Wiki ya Mlipa kodi licha ya kuwatembelea wafanya Biashara katika maduka mbali mbali lakini pia inatarajia kutoa msaada wa kibinaadmu katika hositali ya Abdalla Mzee Mkoani, Pamoja na kutoa misaada kwa familia mbali mbali ambazo zinaishi katika mazingira magumu .
MWISHO
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment