KIONGOZI MWANAMKE ANAEONGEZA KASI YA MAENDELEO KATIKA MKOA WAKE NDANI YA KIPINDI KIFUPI CHA UONGOZI. Uboreshaji wa huduma Muhimu za kijamii ikiwemo Maji, Skuli, Masoko Na vituo vya Afya. Usimamiz bora uwajibikaji i na utayari wa utendaji kazi waelezwa kuchagia kasi hiyo
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA
NI KIPINDI Cha Miaka Miwili ( 2) Tangia Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi Kumteua Salama Mbarouk khatib Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Kushika Nafasi hiyo ambapo Mnamo Siku yaTarehe 1/12/2020 Alimteua Rasmi kushika nafasi hiyo.
Ni Salama Mbarouk khatib ni Mwanamke 1 Pekee alieteuliwa katika Serikali ya Awamu ya nane ya Mapinduzi ya Zanzibar kati ya Wakuu wa Mikoa 5 waliopo Zanzibar ambapo ni sawa na asilimia 20 ya viongozi wote ambao wameshika nafasi hiyo kwa wanawake .
Zanzibar ina jumla ya Mikoa 5 Mitatu kati ya hiyo inapatikana kisiwani Unguja na Miwili iliyosalia ikiwa ipo kisiwani Pemba.
Mabadiliko makubwa yanaendelea kujitokeza katika Mkoa Wa Kaskazini Pemba katika kipindi Kifupi cha Miaka Miwili.
Miingoni Mwa Mabadiliko hayo ni pamoja na Ujenzi wa Matangi ya kuhifadhia Maji, Vituo vya Afya, Skuli, Umeme pamoja na Miundo Mbinu ya Barabara.
Mkoa wa kaskazini Pemba umeundwa na wilaya 2 Wete Na ile ya Micheweni.
Kaskazini Pemba ni moja kati ya Mikoa Miwili ambayo inaongoza kwa idadi kubwa ya watu Zanzibar Kati ya Mikoa 5 ilyopo ambapo kwa mujibu wa Takwimu za Sensa ya watu na makazi Mkoa huo una jumla ya watu 272, 091, Wanaume wakiwa ni 131,484, Na wanawake 140,607, Sawa na Ongezeko la Asilimia 2.3 ukilinganisha na Takwimu za Sensa ya watu na makazi mwaka 2012 ambayo ilikiwa na Asilimia 1.5.
Kwanini Kasi ya Maendeleo katika kipindi kifupi!
" Tunasimamiwa na kiongozi Sahihi ambae ana maono ya Kuifikisha mbali kimaendeleo Mkoa huu, Usimamizi bora wa Majukumu Tuliyopangiwa kufuata sheria, kuendana na kasi ya Mabadiliko Ambayo Dk Mwinyi Rais wa Zanzibar anaitaka Mashirikiano, kutii Maagizo tunayopewa kama wasaidizi wa Serikali, Lakini pia Kupokea ushauri vipi tutaleta mabadiliko katika utendaji ni kitu cha kipekee kwetu. "
Alisema Hamad Omar Bakar ambae pia ni Mkuu wa Wilaya ya Wete.
" Tunapewa Maelekezo na kiongozi wetu Tunafuata Tunafanya kazi kwa Moyo mmoja kusudi tu kuonesha Jamii na Taifa kama kasi ya Mabadiliko sehemu yeyote ile ni utayari wala siyo Jinsia".
" Tunakaa tunatafakari mambo mabli mbali Mazuri ambayo yataleta maendeleo kwa Jamii Yataondosha usumbufu kupata Huduma Bora kwa Wananchi Wetu.
Alisema Mgeni Khatib Yahya Mkuu wa wilaya ya Micheweni.
UPATIKANAJI WA HUDUMA YA MAJI KASKAZINI AWALI NA SASA.
katika kipindi Cha Miaka 3 iliyopita upatikanaji wa Huduma ya Maji Safi na Salama Mkoa wa Kaskazini Pemba Ulikuwa ni asilimia 46 katika Miji na vitongoji vyote ambayo yalikuwa yanapatikana kwa wananchi wote.
Licha ya Hatua mbali mbali kuchukuliwa lakini upatikanaji wa Maji haukuongezeka kutokana na Miundo mbinu kuwa Midogo ambayo hulazimika kutoa Maji kwa Mgao katika Maeneo Mengi ya Mkoa huo.
"Moja kati ya Vitu ambavyo nilivipa kipaumbele kuona vinapata ufumbuzi wa kudumu ni huduma ya Maji kwa Wananchi Wangu ni kutokana na Umuhimu wake hii, Lakini pia nilikuwa najua kwa undani shida hii ilivyo kwa vile nilibahatika kuogoza wilaya za Mkoa huu kabla.
"Kuvuja kwa Pakacha ni Nafuu kwa Mbebaji.
" Kulitolewa Fursa Kusemea changamoto za Mikoa baada ya kuwepo Fedha zile zilizotolewa kwa ajili ya ahueni ya uviko"
"kwa vile ni kitu ambacho kiliniumiza nilitafakari sasa vipi nitalipatia Ufumbuzi suala hili niliitumia fursa hiyo.
" Niliwashirikisha wasaidizi wangu tulipeleka Maombi Kwa Serikali kuu ili tusaidiwe suala hili na Mengine .
Nilifanikiwa Miradi yote ambayo tumeomba imebahatika kutokana na hoja zilizokuwa na Mashiko". Alisema Salama Mbarouk khatib.
SALAMA MBAROUK KHATIB - RC KASKAZINI PEMBA.
"Tuliomba kusaidiwa miradi mbali mbali Elimu, Afya Maji, Barabara, Pamoja na Masoko Kaskazini hatukuachwa nyuma tuliletewa Miradi inayotekelezwa kupitia Fedha za ahueni ya uviko 19 Kiukweli nasubutu kusema Tulupendelewa kuoata miradi Mingi Katika Mkoa wangu.
" Kupatikana Maji kwa Mgao katika baadhi ya Maeneo ndani ya Mkoa wangu ni suala ambalo linanikosesha Usingizi sababu naelewa waathirika wakubwa ni Wanawake na watoto juu ya hili
"Alieleza kuwa Mgao huo umetokana na kuongezeka kwa matumizi na uhitaji wa maji kwa wananchi wake huku Miundo mbinu ya kufikisha maji ikiwa ni Midogo.
"Katika maeneo mengi Visima na Mabomba yanayotumika ni ile iliyowekwa Zamani , na Uhitaji wa Maji ni Mkubwa ukilinganisha na sasa, tunaendelea na kulipatia ufumbuzi suala hilo ikiwemo Ubadilishwaji wa Mabomba kwa kushirikiana na mamlaka yenye dhamana ya kusimamia hili .
Alisema Ujenzi unaendelea huku vikiwa vipo baadhi ya visima ambavyo vilifanyiwa uharaka ili kusaidia kuongeza upatikanaji wa huduma hiyo katika baadhi ya maeneo na vimeanza kutumika.
" Upatikanaji wa Maji katika Mkoa Wangu hadi sasa ni sawa asilimia 54 ambapo awali ulikuwa ni asilimia 46.
Vipo vijiji ambavyo Mgao wake ni kwa uchache Matarajio ni kufikisha asilimia 100 kwa upatikanaji wa maji safi na salama katika miji na vijiji vyote baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Matangi na Visima hivyo.
Suleiman Anass Massoud ni Afisa Uhusiano kutoka mamlaka ya Maji Zanzibar zawa Pemba alisema kuwa Jumla ya Matangi Matatu (3) Visima 11 pamoja na ubadilishaji Mambomba Mapya yenye upana wa nchi 4 na mengine nchi 11 na nusu unaendelea katika Mkoa huo.
" Awali Kaskazini Yote ilikuwa inatumia Tangi 1 na visima visivyozidi vitatu 3 kusambazia Maji, Mabomba ya nchi Moja na nusu Mengine 1 na nusu ndiyo yalikuwa yapo kwa sasa tumebadilisha" .
" Tangi linalojengwa Kilindini Shehia ya Wingwi Wilaya ya Micheweni, Ambalo litakapokamilika litasaidia kuondosha usumbufu huo kwa vijiji vya Shumba Mjini, Majenzi Chamboni na vijiji jirani.
Tangi la Limani Shehia ya Kipange Ambalo linatarajiwa kunufaisha Vijiji vya kipange,Limani, Makangale,Mkia Wa Ng'ombe,Mnarani, Kiuyu Pamoja na Ukarabati wa Tangi la Gando Wete ambalo litakaokamilika litasaidia kunufaisha Vijiji vya Gando Raha, Madaniwa, Mtemani, Mleteni Sambamba na maeneo ya visiwa vya fundo pamoja na uvinje.
VIONGOZI WA SHEHIA WANANSEMAJE JUU YA HILI LINALOENDELEA KWA SASA LA UBADILISHWAJI NA UJENZI WA MATANGI NA VISIMA! .
Rahila Ramadhan Juma Sheha wa Shumba Viamboni Micheweni Pamoja na Mrisho Juma Mtwana Sheha wa Shehia ya Mtemani Wete kwa nyakati tofauti walisema huduma ya maji inayopatikana katika Shehia zao ni ya Mgao jambo ambalo Linapelekea usumbufu kwa wananchi kutokana na kukosa huduma hiyo ipasavyo .
"Tunaona Mabadiliko kuna Mabomba yamelazwa Misingi inachimbwa tunaamini muda si mrefu Maji yatakuwepo, Miaka ya nyuma uo Mgao tulikuwa hatupati walau saivi tunapata kwa Mgao na tunamatarajio ya kupata bila Mgao karibuni.
" Uhitaji wa Huduma za kijamii bila usumbufu si jambo la hiari katika jamii yeyote ile, Idadi kubwa ya watu inapelekea kuongezeka kwa uhitaji na matumzi mengi ya Maji pamoja na huduma nyengine za kijamii.
Shehia yangu Imekombolewa na Wanawake kuna kijijikinaitwa Mleteni kilikuwa hakijulikani kabisa Hakukuwa na Huduma yeyote Muhimu Mpka tuifate mbali lakini kwa Sasa imefunguka kimaendeleo Huduma za Afya zimefika Kwa karibu zaidi na Barabara ipo njiani kuletwa Alisema Shaaban Salum Mtwana Sheha wa shehia ya Kisiwani .
JEE MATUMAINI YA WANANCHI KATIKA USIMAMIZI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA KIONGOZI WAO YAPOJE!
Fatma Ramadhan Said, Safinia Issa Pamoja na Asha Abass ni wakaazi wa Wete walisema hatua hizo zilizofikiwa zimeanza kuleta Mabadiliko ambayo yatapelekea kuboresha huduma za kijamii, kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi pamoja na kuondoa usumbufu wa kufata huduma bora nje ya wilaya hiyo.
"Niseme kuja kwa Miradi hii ya uviko katika Mkoa wetu ni mafanikio bila shaka mpka serikali kuu imeamua kutuletea miradi hii viongozi wetu waliomba kwa nia njema kwetu walipeleka malalamiko bila kupeleka wao sSerikali kuu isingejua kama kuna Matatizo, kwaio tunaimani itakapokamilika tutanufaika sisi na vizazi vyetu.
" Kiukweli tuna matumaini kuona Ujenzi wa hospitali ile ya Micheweni umefikia hatua kubwa sasa umeanza kumaliza itatusaidia sisi akina mama kutuondoshea usumbufu, Mrundikano wa Wagonjwa lakini kurahisisha huduma za Matibabu tunaamini hata huduma ambazo awali tulikuwa tunazikosa mwazo sasa tutazipata ni jambo la furaha.
Sleiman Said Ali ambae ni Mjasirimali Soko la wete
Alisema kuwa matumaini aliyonayo mara baada ya kuona hatua kubwa zilizofikiwa katima ujenzi wa miradi hiyo ikiqemo soko la wajasirimali katika wikaya yake ni makubwa ambapo amesema itasaidia kupata bidhaa kwa urahisi na kwa uhakika pindi atakapozihitaji
KUSHOTO - MJASIRIAMALI WA VIUNGO. SLEIMAN SAID ALI AKIZUNGUMZA NA MWANDISH WA HABARI HIZI.
"Dhamira Njema ya serikali kwa wajasirimali ni kuona tunapata soko la uhakika kuweka na kuuza bidhaa zetu tunaimani kubwa ujenzi wa soko itakapokamilika utakuwa Mkombozi wetu" .
Msimamizi mkuu wa wa miradi ya maenedeleo ambayo inatekelezwa kupitia fedha za ahuweni ya uviko 19 Mkoa wa kaskazini Pemba Amesema hatua iliyofikiwa katika ujenzi wa miradi hiyo itakayotumika kwa wananchi ipo ukingoni kukamilika na kukabidhiwa kwa serikali.
Msimamizi huyo wa ambae ni Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib Alisema uongozi wake utaendelea kutoa mashirikiano yakutosha katika kuona miradi hiyo inakamlika kwa wakati na kutumiwa na wananchi kuleta maendeleo ikiwa na ubora kama matumaini ya wananchi wake yalivyo juu ya miradi hiyo.
Miradi hiyo ni ujenzi wa Masoko ya Wajasiriamali, Skuli Majia miradi ya ujenzi wa Hospitali.
"Wilaya ya Wete eneo la Kifumbi kai, Pamoja na Soko la wajasiriamali Tumbe wilaya Ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba, ambayo hii itakapokamilika wajasiriamlai zaidi ya 154 watanufaika kutokana na kupata sehemu rasmi za kuuza bidhaa zao na kupelekea kuleta tija na ukombozi kwa taifa.
Alieleza kuwa Mradi wa Maji safi na Salama kupitia ujenzi wa Matangi ambao unatekelezwa katika eneo la Kilindini, Wilaya ya Micheweni, Kipange wilaya Wete Sambamba na ukarabati wa tangi eneo la Raha, wilaya hiyo ambapo itakapokamilika miradi hiyo kutasaidia kundoa tatizo la maji katika maeneo mbali mbali.
Aidha Alisema miradi ya Afya inayotekelezwa katika wilaya ya Micheweni ni Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ambapo kukamilika kwa ujenzi huo kutaipa hadhi Hospitali ya Cottage Micheweni na kuwa hadhi ya wilaya Pamoja na ujenzi wa hosptali ya wilaya ya Wete ambao mradi wake unatekelezwa eneo la Kinyasini Wilaya ya wete.
JENGO LA HOSPITALI MPYA YA WILAYA
Hata hivyo Salama alisema Mradi wa mwisho ambao unatekelezwa katika wilaya yake kupitia fedha za uviko 19 ni mradi wa Elimu ambao ni ujenzi wa skuli mpya pamoja na ukarabati wa Madarasa.
"Skuli za kisasa kupitia miradi hii ya uviko ambayo katika Mkoa wangu inajengwa pale Jadida Wete ambayo ni msingi lakini pia Makangale mnarani, awali hazikuwepo u Madarasa mapya, na skuli kisiwa cha kojani, Gando, kiuyu Mbuyuni Matangatuani, Maziwani, sambamba na ukarabati wa skuli za MchinaTumbe Pamoja na Konde
Miradi hiyo ina thamani ya shilingi Bilioni 1. 2 imekamilika kwa asilimia 99 ambapo Kwa mujibu wa Takwimu za Taarifa za Ajira kutoka Taasisi binafsi Mkoa wa Kaskazini Pemba jumla ya watu 1,049 wamenufaika kwa kupata ajira binafsi kupitia ujenzi wa miradi hiyo ya Covid 19 huku vijana wakiwa ni , 410, 234 , kati yao 275 kutoka wilaya ya Wete wanaume 145 wanawake 130, Huku wilaya ya Micheweni vijana 49 wanaume 47 na wanawake 2, Sambamba na Ajira zisizo rasmi 639 ikiwa ni pamoja na kupata utaalamu wa kufanya shughuli mbali mbali, kukuza Biashara na kujipatia kipato katika kipindi cha miaka miwili .
Sio tu Miradi ya Covid ambayo inajengwa na kusimamiwa bali miradi mikubwa ambayo itakuwa fursa kwa wajasirimali Zanzibar.
Tulikuwa na maeneo ambayo ni ya wazi mengi ambayo kwa asilimia kubwa sasa yameanza kutumiwa kueta maendeleo kwa wananchi Tunaendelea na ujenzi wa kiwanda Cha Mwani, Viwanda viwili vya Maji tayari vimeanza kutumika zote hizo ni fursa ambazo zipo katika Mkoa kwa sasa awali zilikuwa hazipo. Alisema Rc
Kuimraika kwa huduma za kifedha Mkoa wa Kaskazini Pemba Ambapo katika kipindi Cha miaka mitano iliyopita huduma hizo zilikuwa ni chache huku baadhi ya maeneo zikikosekana kabisa.
" Kuna tawi la CRDB tunatumia kuhifadhia pesa zetu wengine tumeunga akaunt kupitia hilo tawi zamani tulikuwa hatuna hata io akaunt Fedha zetu zipo salama tunatembea kwa amani bila kuogopa amhaturandi na fedha mifukoni. Aliongeza Sleiman Said Ali.
Wapo Waliodiriki kusema kuwa "Tunatamani Awe na mamlaka ya juu zaidi au ahudumu kwa muda mrefu Mkuu wetu ili tuone Mageuzi mazima ya kiuchumi sio Kaskazini tu Hata Zanzibar Nzima Alisema Zawadi anapambana sana kwajili ya wananchi.
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment