MKUU WA MKOA KASKAZINI PEMBA AKABIDHI MSAADA WA CHAKULA KWA FAMILIA 100 ZENYE HALI NGUMU KANGAGANI AWAHAMASISHA KUDAI RISITI ZA KIELECTRONIKI.
Na AMINA AHMED MOH’D.
MKUU wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib Amewataka wananchi kutoa mashirikiano kwa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB Kwa kudai risiti za kielectroniki wanaponunua bidhaa mbali mbali ili bodi hiyo iweze kukusanya kodi kwa usahihi kutoka kwa wafanya biashara kodi ambazo zitasaidia kuleta maendeleo kwa Wananchi
Ameyasema hayo alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha kangagani katika ghafla ya kupoeana kukabidhi msaada wa chakula uliotolewa na na Bodi ya mapato Zanzibar kwa familia 100 zenye Hali ngumu kijijini humo ikiwa ni Wiki maalum ya kurejesha shukurani kwa walipa kodi nchini.
Amesema iwapo wananchi watatoa mashirikiano na kuunga mkono Ununuaji wa bidhaa kwa kudai risiti za kielektronik kutasaidia kudhibiti upotevu wa kodi na kutumika kodi hizo katika ujenzi wa miradi mbali mbali ya maendeleo unguja na Pemba na kutumika kwa maslahi ya Taifa .
Awali akizungumza Mkurugenzi wa ZRB Pemba Jamal Hassan Jamal amesema msaada huo uluotolewa na bodi hiyo ni katika kurejesha shukurani kwa walipa kodi ambao ni wananchi .
Nao baadhi ya wananchi wa kijiji hicho wameishukuru ZRB kwa kuwapatia msaada huo ambapo wamewataka kuendeleza Utamaduni huo wa kuwakumbuka walipa kodi wao ambao wanaishi katika Mazingira Magumu maeneo mbali mbali.
Msaada uliotolewa kwa wananchi hao ikiwa ni wiki ya furaha na kurejesha shukurani kwa walipa kodi ni Sukari, Mchele, Unga pamoja mafuta ya kupikia ambapo mapema asubhi wafanya biashara mbali mbali waliofika katika ofisi za bodi hiyo Gombani chake chake walijmuika pamoja na wafanya kazi wa bodi hiyo katika shehehe maalum ya kuwashukuru walipa kodi .
Mwisho
Comments
Post a Comment