MWAKILISHI JIMBO LA BUBUBU WAJADILI MIRADI YA MAENDELEO NA WANANCHI WAKE.
NA MWANDISHI WETU UNGUJA.
UKUSANAYAJI wa maoni kwa wananchi wa jimbo la bububu utasaidia kujuwa aina ya miradi itakayowanufaisha wananchi kimaendeleo
Hayo yamebainishwa na Mwakilishi wa Jimbo la Bububu Mhe Mudrik Ramadhan Soraga baada ya mkutano wake na wananchi wa jimbo hilo ili kukusanya maoni ya wananchi kuhusiana na miradi wanatohitaju kutekelezewa huku shehia ya bububu Wilaya ya Magharib A Unguja.
Amesema ziara hizo zimekuwa zikifanyika mara kwa mara ndani ya jimbo lake kupitia kamati yake zenye lengo la kuibya miradi itokanayo na maoni ya wananchi kwa ajili ya utekelezaji ili kuboresha maisha ya wananchi ikiwemo wazee, vijana na watoto ndani ya jimbo hilo
Ameongeza kuwa kufuatia maoni waliyoyakusanya kutoka kwa wananchi hao kamati yake itayachukulia kwa umuhimu mkubwa na anaamini yatasaidia kutekeleza ahadi alizoahidi wakati alipokuwa akiomba nafasi hiyo sambamba na kuomba mashirikiano ya wananchi katika utekelezaji huo
“Kupitia maoni haya naamini tutaibua miradi miwili mitatu ambao tutaifanya kwa ufanisi na naamini wananchi watafurahia matunda ya kiongozi wao” alisema Soraga
Kwa upande wake Rahma Haji Ameir mwenezi wa wadi ya Bububu kupitia CCM amesema wamefirahishwa sana na ujio wa kiongozi huyo ambapo kwa upande wake amependekeza mradi wa kujengewa kituo cha mafunzo ya amali itakachowawezesha vijana kujifunza fani mbali mbali ikiwemo ushoni, uchoraji ili kujitengenezea ajira na kuacha kufikiria ajira kutoka serikalini
Nae sheha wa Shehia ya Bububu Suelum Ali Juma amesema mkutano huo umekwenda vizuri na amewashukuru wananchi kwa kushiriki vyema mkutano huo na kutoa maoni na mapendekezo yao yatayosaidia kupata miradi yenye matarajio makubwa ya kuwafusaisha wananchi wa jimbo hilo na taifa kwa ujumla.
Ziara hiyo yenye lengo la kukagua utekelezaji wa miradi pamoja na kuibua miradi mipya itakayotelelezwa kupitia mfuko wa Mwakilishi imeanzia shehia ya Mbuzi na bububu na inatarajiwa kuendelea tena katika shehia zote za jimbo hilo
Comments
Post a Comment