Zoezi la Usafi Hospitali ya Chake Chake

Na AMINA AHMED    
MKUU wa Wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali  leo ameongoza zoezi la  ufanyaji wa usafi katika hospitali ya wilaya Chake Chake lilioandaliwa na Bodi ya mapato Zanzibar ZRB ikiwa ni muendelezo wa mwezi wa kurejwsha shukurani kwa mlipa kodi. 

Akizungumza   na watendaji wa ZRB mara baada ya kumalizika kwa zoezi hilo Mkuu wa Wilaya huyo Amesema kuwa suala la usafi katika Hospitali lina umuhimu mkubwa kwa afya ya wagonjwa, wauguzi na watu wengi wanaofika katika maeneo hayo . 

Amesema kuwa   kuwepo kwa mazingira safi  kutasaidia kupatikana afya  bora kwa wananchi ambao wao ndio walipaji wa kodi zinazosaidia  kuleta Maendeleo. 


Mapema Mkurugenzi wa Bodi ya Mapato Zanzibar ZRB  Pemba Jamal Hassan Jamal amesema ZRB itaendelea kuunga mkono upatikanaji wa huduma bora za kijamii kupitia kodi wanazolipa kwa kurejesha shukurani.


Kwa upamde wake Daktari dhamana Hospitali ya Chake Chake Dr. Abrahman Said Mselem ameushukuru uongozi wa ZRB kwa uamuzi wa kufikia na kusaidia shughuli za usafi Hospitali hapo ambapo amzitaka taasisi nyengine kuiga mfano huo .

Zoezi hilo  ni muendelezo wa shamra shamra  za mwezi wa mlipa kodi ambapo awali shughuli mbali mbali za kimaendeleo zimefanyika ikiwemo kusaidia vifaa   vya matibabu katika hospital mbali mbali,   vyakula kwa watu wasiojiweza, kuzungumza na wafanya biashara kusikiliza chamgamoto zao,  na kutoa elimu kwa wafanya biashara katika maduka mvali mvali kusini na kaskzini Pemba.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI