Watumishi wa umma wapewa neno
WATUMISHI WA UMMA WAMETAKIWA KUFUATA MUONGOZO NA KANUNI ZA KAZI KATIKA UTEKELEZAJI WA KAZI ZAO ILI KURAHISISHA SHUGHULI ZA KUKUZA ZA MAENDELEO NA KUPELEKEA KUIMARIKA KWA UKUAJI WA UCHUMI NCHINI.
AKIZUNGUMZA WAKATI AKIFUNGUA MAFUNZO KWA WATENDAJI WA AFISI YA RAISI KAZI UCHUMI NA UWEKEZAJI HUKO UKUMBI WA AJIRA WA OFISI HIYO MWANAKWEREKWE KAMISHNA WA KAMISHENI YA KAZI RASHID KHAMIS OTHUMAN AMESEMA MABADILIKO HAYO YANAWEZA KUFIKIWA KWA HARAKA ENDAPO KUTAKUWEPO NA MASHIRIKIANO YA PAMOJA BAINA YAO
AMESEMA KUWA NI VYEMA KWA KILA MTUMISHI KUHAKIKISHA ANATEKELEZA WAJIBU WAKE ILI KUONA MALENGO YA SERIKALI YA KUWA NA WATUMISHI BORA YANAFIKIWA NA KULETA MAFANIKIO
HIVYO AMEWWTAKA WAFANYAKAZI HAO KUJIFUNZA ZAIDI KATIKA MASUALA YA SHERIA ZA KAZI HATUA AMBAYO ITASAIDIA KULETA MATOKEO MAZURI HAPO BAADAE NA KUJENGA UFANISI
AMESEMA NI WAJIBU KWA KILA MTUMISHI KATIKA SEKTA YA UMMA KUFAHAMU MAJUKUMU YAO KISHERIA NA KUHAKIKISHA ANATEKELEZA KWA KUFUATA MIONGOZO ILIOPO SERIKALINI ILI KUEPUSHA UBABAISHAJI
Comments
Post a Comment