TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SKULINI, BILA HUDUMA YA MAJI, DAMPO NA VYUMBA MAALUM HAKUNA HEDHI SALAMA,NI HATARI KWA AFYA ZAO NA ATHARI KATIKA UFAULU WAO.
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. ( 0719859184) IKIWA JANA 28 /5/ Dunia iliaadhimisha siku ya Hedhi Salama bado kuna mengi yanahitaji kuangaliwa na wadau Serikali na wote wanaopenda Maendeleo bora ya Elimu kwa watoto wa kike kwa Shamra shamra mbali mbali ikiwemo kutoa Elimu ya Afya ya uzazi kwa baadhi ya wanafunzi, kugawa Sabuni pamoja na Taulo zakike lakini bado kuna changamoto Nyingi ambapo zisipoangalia kwa jicho la Tatu na wadau pamoja na serikali kwakuwekewa mkakati Endelevu Kugawa Taulo kutoa Elimu na Sabuni hizo hautokuwa Msaada kwa Wanafunzi Wakike Maskulin i. Jee ni kwa namna gani yataweza kufikiwa Maendeleo ya Elimu ambayo itakuja kuwa mkombozi baadae katika maisha ya mtoto wa kike ni pamoja na kuwa na Afya imara mazingira salama na upatikanaji wa huduma muhimu ambazo zitasaidia kuondosha usumbufu wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi. Wanafunzi wengi wakike ambao wamefikia umri wa baleghe ( kuvunja ungo) wakiwa katika hara...