WANANCHI PEMBA WALIA KUKOSA HUDUMA YA MAJI SAFI NA SALAMA WAOMBA WADAU NA SERIKALI KUJITOKEZA KUWASAIDIA, WADAI KUKOSA MATUMAINI NA AHADI WANAZOPEWA NA ZAWA.

Na Amina Ahmed Moh’d, Pemba- (0719859184)

BAADHI YA WANANCHI   Shehia ya Gombani wilaya Ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba Wamemuomba Waziri wa Maji  , nishati na Madini, Zanzibar Shaib  Hassan kaduara kulipatia Ufumbuzi Tatizo la ukosefu wa Huduma ya Maji Safi na  Salama  katika Baadhi ya Vijiji ndani ya Shehia yao kwa Muda mrefu sasa ambalo limeshindwa kupatiwa ufumbuzi. 

 Wakizungumza na Habari hizi  baadhi ya wakaazi wa Gombani Wamesema kukosa huduma hiyo kwa muda mrefu   sasa bila muelekeo wa kuoatikana ufumbuzi tatizo hilo imekuwa  kukirudisha nyuma Matumaini yao katika kuipata huduma hiyo muhimu.

" Tunawaomba wahisani wanaowajengea  Visima watu vijijini waje na Shehia ya Gombani wasiwekeze tu Vijijini,  tunausumbufu mkubwa kwa Muda mrefu sasa waje watusaidie, au Waziri mwenye dhamana  Kaduara  asilichukulie masihara hili suala Wananchi wake tunasumbuka sana na  Watoto, kila siku tunaambiwa kuna matenengezo wala hayamalizi  tumekuwa tunadanganywa kama  watoto wa kuku". 

 " Shehia ya Gombani ni Moja Lakini chakushangaza Baadhi wanapata Maji wengine wanakosa, mwaka huu sasa kama sio mwaka wa Pili, Mimi mtoto wangu kazaliwa ana  Mwaka hajawahi kuona maji ya ZAWA Tumechoka kupiga kelele kila siku", Alisema Ilham Salum Mkaazi wa Gombani. 

 "Hatujui hata izo kero Tuzitolee wapi  haswa mana kama ni kwenye Vyombo vya Habari tumetoa Mpka kwenye Mawio lakini hakuna mabadiliko yoyote, Mkija kutuhoji tunaona kama mnatujejea  sababu hakuna kinachobadilika  Maji hayatoki mifereji imeshashajiloki yenyewe, Alidai Sadam Omar. 

" Mwaka huu kama sio mwaka Wa Pili mi sijaona maji kwangu wala kwa Majirani tunastiriwa na wale  wasamaria wema wenye kisima chao Ndani kama sio hivyo ingekuwaje sijui “Alisema Latifa Ali Hamdan. 

 Akizungumzia Suala hili Sheha wa shehia ya Gombani wilaya ya Chake Chake Subira Khamis Kombo  Alidai kuwa Upatikanaji wa Maji  safi na salama katika shehia yake Umekuwa  na ahadi  zisizotekelezeka kutoka mamlka ya maji Zawa. 

 "Kusema kweli ndugu Mwandishi  Gombani Maji ya uhakika bado hatuna  najitahidi kufuatilia Suala hili lakini majibu  yanakuwa yale kwa yale tu  kutoka kwa mamlaka husika,  huku Tatizo likizidi kuwa kubwa  na la muda Mrefu, Wito wangu kwa Serikali kuu  iangalie Muarubaini wa hili, wahisani pia wajitokeze kutusaidia, ili na sisi tuweze kupata Maji kama vijiji vyemgine. 
 
 Harakati za Kumtafuta Msemaji wa mamalka ya Maji Zanzibar zawa Ofisi ya Pemba juu ya Kuzungumzia Suala hili kwa mara ya Tatu zinaendelea, ambapo awali mnamo 

msemaji huyo ambae ni Afisa Mahusiano mamlaka ya Maji zaaa Pemba Suleiman Anas Massoud Alizungumza na habari hizi kwa niaba ya Mkurugenzi wa  Mamlka ya Maji Zanzibar Zawa Ofisi ya Pemba ,   na kuwataka  Wananchi  Hao wa  Shehia ya Gombani kuendelea kuwa Wastahamilivu  kwani Mradi  utakaonufaisha Upatikanaji wa Huduma ya Maji vijiji   Vya Gombani Umefikia Hatua Nzuri. 
 
"Matarajio Yetu  tulikusudia  Mwanzoni Mwa Mwezi huu Tatizo la Maji baadhi ya Vijiji Gombani libaki Historia tu Lakini Kutokana na Sababu zilizokuwa Nje ya Uwezo Wetu  Mradi huo Utamaliza Mwisho wa Mwezi wa March Mwaka huu 2023.

Anass Alitaja  Sababu hizo  na Kusema kuwa " Baadhi  ya  vifaa vyao Vya Ujenzi na ulazaji Mabomba Vilizuiwa Bandarini Unguja  Kwa hiyo Mafundi wakachelewa  Vilikuwa havitoshi kukamilisha kwa wakati Mradi, Mabomba, Viungo, Pampu, Saruji, Kokoto, Nondo, na Magari ya Kukorogea Zege" Alisema. 

Akizungumzia Suala la Utolewaji Taarifa kwa Wananchi juu ya Hatua za Ujenzi wa Mradi  huo   Sleiman alisema kuwa Mamlaka ilitumia vyombo vya Habari mbali mbali kuwajulisha wananchi. 

" Hatukumfata kila Mtu kwake lakini katika Media ZBC Redio Tv, na Radio Jamii na baadhi na Vikao vya Masheha Wilaya zote Tumewambia nini kinaendwlwa kwa sababu Mradi wa Maji Gombani ni moja kati ya miradi  inayotekelezwa kwa Fedha za ahuweni ya Uviko 19.

Aidha alisema kuwa Mamlaka imelenga kuimarisha Huduma ya Maji kwa kuongeza idadi ya Visima vya Maji vitakavyo Hudumia Chake Chake ikiwemo Gombani. 

Kwa Mujibu wa Sheha wa Shehia ya  Gombani jumla ya  Wakaazi 4835 ambao wao ni Wanawake na Watoto wamekuwa wakishindwa kufanya shughuli zao kwa wakati kutokana na usumbufu  wa kukosa Maji  baadhi ya Maeneo. 

Ambapo kwa Zaidi ya Miezi Saba Sasa na hulazimika kuyafata Masafa ya mbali   huku baadhi ya Maeneo kupata kwa Mgao usiku usiku ambapo Mnamo siku ya Tarehe 16/12  2022 Uongozi wa Mamlaka  ya Maji Zanzibar zawa ofisi ya Pemba walidai kuwa Suluhu ya Usumbufu huo itakamlika Mwanzoni mwa Mwezi 12 2022, kutokana na kuendelea kwa ujenzi wa mradi  visima pamoja na Ukazaji wa Mabomba yakusambazia Maji jambo ambalo limeshindwa kukamilika. 

Mwisho 


 

 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI