UONGOZI WA MGENI KHATIB YAHYA UNAVYOENDELEA KUACHA ATHARI KATIKA KIPINDI KIFUPI , AWATAKA WANAWAKE KUACHA WOGA NA WAJITOSE KUTAFUTA UONGOZI ASEMA WAO NDIO CHACHU KUBWA YA MAENDELEO KWA TAIFA.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA
Moja kati ya Majukumu Makubwa ni Uongozi, Uongozi ni hali ya Mtu mmoja kuweza kuewa nyazifa ya juu kuongoza Kundi la watu taasisi, Ambapo mtu huyo hupewa mamlaka ya kufanya maamuzi katika kuleta Maendeleo.
"Dhana hiyo ya Uongozi wenye kuleta Maendeleo kwa Miaka mingi imejengeka akilini mwa waliowengi kuwa Mtu sahihi ambae anaweza kuleta maenedleo ni mwanaume pekee jambo ambalo halina ukweli wowote ule kikubwa kinachohitajika ni utayari na uwajibikaji tu juu ya kile kinachoongozwa na sio jinsia kama wanavyodhani wengi".
Ni maneno ya Mkuu wa Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba Mgeni khatib Yahya alipata ku uteuzi wa nafasi hiyo ya kuongoza na kusimamia wilaya kutoka kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi Huku akiwa ni Miongoni mwa Wanawake wachache waliteuliwa kushika nafasi hiyo.
Licha ya uongozi huo wa Wilaya , Mgeni Khatib pia ni mama wa Familia lakini pia na nk Mke ambae Anasimamia vyema majukumu yake kama mke na mama kwa watoto wake.
Yapo mengi Mazuri ya kuigwa na Wanawake wengine ambao wana malengo ya kuwa viongozi katika nyazifa mbali mbali za uongozi ikiwemo, uwajibikaji kupambana kutimiza malengo ya Maendeleo kwa jamii, kuishi vyema na jamii lakini na kutimiza malengo na ndoto ambazo wanawake wengi wamekuwa wakijiwekea.
Mgeni khatib yahya licha ya kuwa ni Mkuu wa wilaya ya Micheweni lakini Pia Aliwahi kuwa Mkuu wa wilaya ya Wete Kaskazini Pemba ambae ni Mtoto Wa sita kuzaliwa kati ya watoto Saba Kutoka kwa Familia ya Mzee Khatib Yahya.
Kama hiyo haitoshi harakati zake za Uongozi zilianza muda mrefu mpka kufika hapo Alipo sasa huku akidai kuwa siri kubwa ni kutokata Tamaa.
ALIANZAJE HARAKATI ZA UONGOZI MPKA LEO MKUU WA WILAYA
Mgeni Khatib kwa Sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Micheweni, ambapo katika Awamu ya nane Mwanamke Ametumikia wilaya mbili kwa nyakati tofauti ndani ya Mkoa wa kaskazini Pemba, Aidha kabla ya Kuwa Mkuu wa Wilaya Mgeni Khatib Aliwahi kuwa Mwalimu katika Skuli ya Jadida, Utaani, Pamoja na Kizimbani ambapo alizaliwa Katika Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba na kusoma Elimu yake Ya Msingi na Sekondari katika Skuli ya Miti Ulaya PA momoja na Utaani kabla ya kuendelea na harakati zake za kutafuta Elimu ya juu kisiwani Unguja.
Akiwa Mwalimu Alindelea na harakati za Masomo katika Chuo kikuu cha Zanzibar University Katika fani ya Ualimu, Na baada ya Muda Kubadilisha Fani ya ualimu hadi kusomea fani ya Biashara na Masoko ambapo fani hiyo ilipelekea kubadilisha kutoka kuwa mwalimu na mfanyakazi wa wizara ya Elimu hadi kuwa Afisa Masoko katika Wizara ya Biashara Zanzibar.
JEE DC MGENI ALIFIKAJE KUWA KAIMU TUME YA USHINDANI HALALI WA BIASHARA ?
Safari Ya kuwa kiongozi ilianza pale ambapo Wizara ya Biashara ilipoanzisha Tume maalum ya ushindani halali wa Biashara na Ndipo Mkuu huyo alipoanza kupata nafasi ya kuwa kaimu Mratibu wa Tume hiyo na kubahatika kuongoza kwa Muda mpka mwanzoni mwa mwaka 2020.
Akiwa katika harakati za Ualimu Dc Mgeni pia alikuwa mwanaharakati katika masuala mbali mbali ya Maendeleo ndani ya Chama cha Mapinduzi ambapo suala hilo lilimpelekea kuhamasika na kugombania nafasi za Uongozi wa Majimbo huku dhamira yake kubwa ikiwa ni kuwa msaada kwa jamii yake iliyomzunguka katika kuleta Maendeleo ,
Ambapo Mgeni Khatib aligombea nafasi mbali mbali za ndani ya Chama hadi kupata uthubutu wa kugombea nafasi ya Ubunge mwaka 2020 Jimbo la Mtambwe Mkoa wa Kaskazini Pemba Kupitia Chama cha Mapinduzi CCM jimbo ambalo lilikuwa na upinzani Mkubwa huku wapinzani wote walioligombania jimbo hilo kuwa ni wanaume .
"Chama changu cha Mapinduzi kiliniamini, nakunipatia nafasi ya kuingia kugombania Ubunge jimbo la Mtambwe, na niliweza kusimamisha vizuri bendera ya chama kwa kuchuwana vikali na wenzangu bahati haikuwa ya kwangu kura hazikutosha nilikosa kuwa mbunhe jimbo hilo lakini sikukata tamaa, Niliendelea kukitumikia chama changu kwa moyo mmoja huku nikiendelea na kazi yangu na kukaimu nafasi katika wizara ya Biashara.
Baada ya Uchaguzi kumalizika nikiwa bado ni mfanya kazi wizara ya biashara nilipata Uteuzi kutoka waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ wa Kuwa Diwani wa kuteuliwa na kweli nilikuwa diwani wa kuteuliwa wakati huo huo naendelea kuwa kaimu wa tume ya ushindani halali wa Biashara na kumlinda Mtumiaji Pemba.
Haikuishia hapo harakati za kutafuta uongozi ziliendelea
baada kuwa Diwani wa kuteuliwa Ikafika zamu ya kugombania nafasi ya Mwenyekiti pamoja na katibu ambae ataweza kuongoza madiwani wote Ndani Wilaya ya Wete Dc Mgeni hakusita kulenga shabaha yake Kuomba nafasi hiyo.
"Niliomba kura kwa Madiwani wenzangu kugombea nafasi ya uwenyekiti wa Madiwani na nilishinda na hatimae kuwa Mwenyekiti wa Madiwani Baraza la Mji Wete.
" Nilibahatika kuongoza nafasi hiyo kwa kipindi kifupi sana cha mwezi Mmoja na nusu tu na hapo ndipo namshukuru Mh Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi aliponiteuwa kwa mara ya kwanza kuwa Mkuu wa wilaya ya Wete.
Ni Maneno ya Mkuu wa wilaya ya Micheweni Mgeni khatib OK yahya.
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni huanza vyema Siku yake Kwa Kuamka Mapema Na kufanya Mazoezi ambapo hutumia takriban Kilomita 4 kukimbia kila siku ili kuimarisha afya ya mwili wake jambo ambalo Hutumia kama mfano wa kuhamasisha wananchi wa wilaya yake anaowaongoza.
Lakini pia kutembelea Wakulima, Wagonjwa Hospitali ni miongoni wa Tabia ambazo zimejengeka kama utamaduni wake wa kufata moja kati ya siku za Katika Wiki.
SERIKALI YA AWAMU YA NANE
Mnamo Disemba 28 mwaka 2020 Harakati za Uongozi wa kuteuliwa kwa Mwanamke huyo kuwa Mkuu wa wilaya zilisikika katika Vyombo mbali mbali vya Habari ambapo Rais wa Zanzibar wa Awamu ya Nane Dk Hussein Ali Mwinyi Alipoteuwa Wakuu wa wilaya 10 za Zanzibar Huku Mgeni Kuwa mmoja kati ya Wakuu hao na kuteuliwa Kwa mara ya kwanza kuongoza nafasi hiyo ya juu ya Uongozi na kuwa Rasmi Mkuu wa wilaya Ya Wete .
Anasema kwa mara ya kwanza alihisi Ugumu kwa kua hakua mzoefu, Wala hakutarajia kupata nafasi hiyo, lakini kadri siku zilivyosonga mbele alizidi kuwa bora zaidi, na hilo ni kutokana na vitu alivyopewa kusimamia kwenda vizuri na kufanya kazi kwa utayari kwa kufuata misingi ya kisheria.
Licha ya kuwa Mpya katika Teuzi Alisema hakuwa na ugeni katika utendaji, baada ya kupata maelekezo katika majukumu yake na alifanya wajibu wake katika nafasi hiyo kwa vilealiwahi kuwa mtendaji katika nyazifa nyengine kabla ya kupata nafasi hiyo kubwa
Mwanamke hana Ugeni Popote , pia mama, Mwalimu pia ni kiongozi, niliendeleza ujasiri wa kufanya kazi vizuri kama ninavyoisimama majukumu ya Familia yangu na kule ambako nimetoka kwa Mashirikiano.
ALAMA ZA UONGOZI BORA NA MAENDELEO ZILIZOACHWA NA DC MGENI .
Mkuu wa Wilaya ya Micheweni aliweza kuongoza Wilaya ya Wete kwa kipindi cha Miezi 8 Pekee kabla ya kuongoza Wikaya ya Micheweni lakini Alama za Utendaji kazi wa kuketa mageuzi ya maendeleo uliochwa katika wikaya hiyo hautosahaulika kwa baadhi ya vijiji ambavyo kwa Jitihada na umakini wa kiongozi huyo aliuonesha.
Mleteni, Tondooni,na vijiji Jirani ni moja kati ya Vijiji ambavyo vilikuwa na usumbufu mkubwa wa huduma za Maji safi umeme barabara pamoja na vituo vya afya katika kioindi kifupi cha Uongozi huo Shida hizo zilianza kuoata ufumbuzi.
Anapokuwa katika utekelezaji wa Majukumu yake ya uongozi Dc Mgeni hulazimika kutenga Muda maalum kuzungumza na wananchi wanaofika ofisini kwake kwa kusikikiza shida changamoto na mawazo mbali mbali jambo ambalo limepikelewa na kuongelewa kama Hadithi njema kwa wananchi wa Micheweni.
WANANCHI WANASEMAJE.
" Kijiji Chetu cha Mleteni hatukuwa na imani kabisa juu ya kupata Maendeleo ya aina yeyote ile Tunashukuru Awamu ya nane ilipomteuwa mama yetu Bimgeni Ndio alikuwa kama ufunguo wetu wa maendeleo Alikuja tukamueleza mambo mbali mbali na tunashukuru alileta Mpka kiongozi wa nchi kuja kujionea kero zetu na zinaendelea kupatiwa ufumbuzi Mpka leo licha ya kuwa yeye kaondoka.
Tunamkumbuka kwa Mazuri Huduma za afya hazikuwepo kabla yake Tatizo la maji safi ndio lilikuwa pasua Kichwa Mleteni Tunamkumbuka kwa wema kunakuja Miradi mbali mbali yakufungua maendeleo.
Ni Maneno ya Muhammed Omar Said na Saade Salumu (Mama nai) wa kijiji Cha Mleteni.
Nassor Ali Ni mjasiriamali kutoka kikundi cha Jitihada Wilaya ya Micheweni Anasema Sio tu ni kiongozi bali ni Mama ambae anajenga matumaini kwa vijana katika Kufikia maendeleo.
"Amekuwa akitusapoti Sisi wakulima wa tulikuwa hatuna soko katusaidia, anapokuja hapa anakuja kama mtu wakawaida huwezi kuamini kama ni kiongozi anashika jembe analima anatupa mawazo mazuri ya kibiashara,Kusema kweli Mama amekubalika kwa sababu anajuwa kuishi na jamii yetu.
Fatma Ramadhan Bakari Mkufu Issa na Asha Abdi Juma ni wakaazi wa Wilaya hiyo, walisema hatua zilizofikiwa na Mwanamke huyo zimeanza kuleta mabadiliko ambayo yanaboresha huduma za kijamii, kukuza maendeleo ya kiuchumi kwa wananchi pamoja na kuondoa usumbufu wa kufata huduma bora nje ya wilaya hiyo na Kuimarisha harakati zao mbali mbali.
KUNA TOFAUTI ILIOPATIKANA KATIKA MAENDELEO AWALI NA SASA KATIKA WILAYA HIYO! .
Wilaya ya Micheweni ni moja kati ya Wilaya ambazo zimakuwa na harakati nyingi katika Sekta ya Kilimo, biashara Pamoja na Uvuvi ambapo kwa Asilimia kubwa harakati hizo huendeshwa na Vijana pamoja na wanawake.
"Kama nilivyokueleza awali Ndugu Mwandishi nimesoma pia mambo ya Biashara na nina Degree kwaio sikai tu bure bure nimekua nikitumia iyo elimu kuwasapoti vijana namna bora ya kuanzisha biashara waweze kujikwamua kupitia kilimo chenye tija".
kama hiyo haitoshi Mimi pia nimewahi kuwa mwalimu naendelea kusimamia Mendeleo ya elimu kupambana na utiro kwa kushirikiana na wananchi na wizara, Na kwa vile niliwahi kuwa mwanasiasa niko bega kwa bega na mshauri katika maabaraza ya vijana kuona tunatoa ushauri wa mambo mbali mbali ya maendeleo kwa vijana na wanawake ikiwemo hili la Uongozi.
Harakati za kinamama kuimarika zikiwemo za ufinyanzi, ushoni na usarifu wa bidhaa kwa kushirikiana katika kutatua Changamoto zinazowakabili ikiwemo uoatikanaji wa soko.
Kusimamia malezi ya pamoja kudhibiti mmonyoko wa maadili kwa vijana walichini ya umri wa miaka 18 kwa kushirikiana na wazazi sambambana jeshi la Polisi.
Jambo jengine alilofanikiwa Mwanamke huyo ni kusimamia ujenzi wa spitali ya wilaya katika eneo la Majenzi , pia usimamizi wa skuli mbali mbali ikiwemo skuli ya Mnarani makangale , ambayo imewakilisha vizuri suala la elimu katika wilaya hiyo .
CHANGAMOTO ALIWEZAJE KUZIFANYA KUWA FURSA YA KUFIKIA HAPO ALIPO SASA!.
"Napenda sana kujifunza kwa wengine ambao ni viongozi mambo mazuri nimekuwa nikipokea Ushauri kwa kiongozi wangu wa mkoa na kuiga pia mazuri yake ya utendaji ".
"Nimeweza kushinda changamoto sababu kubwa ni kuwa tayari na kuamini kwamba changamoto haziepukiki Zipo nyingi tu lakini naendelea kuzishinda. Alisema Mgeni" .
DC MGENI ANASEMA FAMILIA SIO KIKWAZO BALI NI DARAJA LA KUFIKA HAPO ALIPO SASA.
Nikiwa kama mama Na mke pia Mumewangu Ni msaada mkubwa katika harakati zote hizo nilizopitia Nakumbuka kipindi nagombea nafasi wakati napita kuomba kura nilikuwa natumia usafiri wake yeye ndio ananiendeshea ananisubiri na kila nilipohitaji sapoti alikuwa mstari wa mbele, na hadi sasa anaendelea kunisapoti katika kuona nasimamia vyema majukumu yangu.
MALENGO YAKE NI YAPI KATIKA KUENDELEZA SIFA ZA KUWA KIONGOZI BORA ZAIDI WA TAIFA HILI KUHAMASISHA WENGINE NA JEE ANA WITO GANI KWA WANAWAKE WENGINE.
"Tunasimamiwa na kiongozi mwenye maono ya kuibadilisha Zanzibar sambamba na kuendana na kasi ya mabadiliko kwa kuzingatia mashirikiano hivyo naendeea , kutii maagizo kama msaidizi wa Serikali, pia kupokea ushauri namna ya kuleta Mabadiliko katika utendaji ambayo yataleta Maemdeleo zaidi kwa wananchi na Taifa "
" Wanawake Tunaweza sna Asilimia 100 tulikuwa tunarudishwa nyuma kuonesha uwezo wetu kutokana na mfumo Dume kwa Miaka Mingi Lakini sasa ni muda wa kuamka kuomesha Dunia uwezo wetu katika kuleta Maendeleo".
Shughuli za Familia hazisababishi mwanamke kushindwa kuwajibika anapopewa uongozi anaweza kuwajibika bila kuathiri familia wala uongozi hivyo Msiogope Tuendelee kujitokeza kuonesha uwezo wetu kwa kutenda mazuri tunapopata nafasi.
Kama ambavyo Rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi alivyoonesha kuwa na imani na wanawake kwakuwashirikisha katika nafasi mbali mbali tuendelee kumpa imani azidi kutuamini na kuongeza idadi katika nafasi za juu za uongozi.
Ni Busara za Bi Mgeni Khatib kwa Wanawake Zanzibar kuelekea 20 -25
KATIBA YA ZANZIBAR INASEMAJE JUU YA WANAWAKE KUWA VIONGOZI.
Kwa mfano katiba ya Zanzibar ya mwaka 1984, katika kifungu 21(2) kila mzanzibari anayo haki na uhuru wa kushiriki kwa ukamilifu katika kufikia uamuzi juu ya mambo yanayomuhusu na yanayohusu taifa lake.
DIRA YA ZANZIBAR 2050 INATAKAJE JUU YA UONGOZI KWA WANAWAKE.
Aidha Dira ya Zanzibar katika maazimio ya 2.5.1 hadi 2.5.9 yameeleza masuala mbali mbali ya usawa wa jinsia na kuondoa unyanyasaji wa kijinsia pamoja na kuimarisha mifumo ya uwezeshaji wanawake ikiwemo kuinua na kutoa nafasi za uongozi kwa wanawake katika jamii.
Pia kuongeza fursa na kuwawezesha katika vyombo vya kutolea maamuzi na kwenye shughuli za uchumi, kijamii, siasa katika ngazi zote za utawala na huduma za sheria.
WANAWAKE KUONGOZA KWA MUJIBU WA SHERIA
Kwa mujibu wa Katiba Ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ya Mwaka 1977,Ibara ya 5(1) mtu yeyote bila kujali jinsia (mwanaume au mwanamke) mwenye umri pm usiopungua miaka 18 ana haki ya kuchagua au kuchaguliwa kuwa kiongozi (Ibara ya 5(1).
Mwisho
Comments
Post a Comment