WANAFUNZI MADUNGU SECONDARI WAIPONGEZA TAASISI BAREFOOT COLLEGE INTERNATIONAL ZANZIBAR, KWA KUWAFANYIA MAZURI HAYA KUELEKEA SIKU YA HEDHI SALAMA , HUKU WAKIIBUA MENGINE YANAYOHITAJI MSAADA KATIKA KUIMARISHA AFYA ZAO NA KUTIMIZA MALENGO YAO WALIYOJIWEKEA. .
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA (O719859184).
KILA Ifikapo May 28 Dunia huadhimisha Siku Ya Hedhi Salama Ambapo Katika kuadhimisha Siku hiyo Wanafunzi Wa Skuli ya Sekondari Madungu wameishukuru Taasisi ya Barefoot College International Zanzibar kwa kusherehekea siku hiyo Pamoja nao kwa kuwapatia Elimu ya Afya ya uzazi kwa Mwanamke sambamba na kuwagawia Taulo za kike, Nguo za ndani, pamoja Sabuni ya Unga ambapo Wanafunzi hao wamewataka wadau wengine kuendelea kusaidia upatikanaji wa Elimu na vifaa hivyo ili kuimarisha Afya za watoto wakike katika Maskuli mbali mbali Mijini na Vijijini na kuwaondoshea usumbufu.
Wakizungumza mara baada ya Kumalizika kwa Zoezi la utolewaji wa Elimu hiyo ya Afya, Ugawaji wa Taulo hizo Nguo za Ndani pamoja Sabuni Baadhi ya Wanafunzi hao wamesema iwapo Wadau kutoka taasisi na Mashirika Mengine wataungana pamoja na Taasisi ya Barefoot kutasaidia kuwaondoshea usumbufu wanaokumbana nao watoto wakike wengi ambao kutokana na kukosa Elimu na Hifadhi Wanapokuwa katika kipindi hicho hupelekea kudhorota kwa ufaulu wao.
"Tunaishukuru Taasisi ya Barefoot kwa Kuona umuhimu wa kutoa Elimu hii kwetu sisi watoto wakike, Mengi tumeweza kujifunza kupitia Siku hii ya leo ambayo tulikuwa hatuyajui, Tunaomba na wadau wengine wajitokeze kwani uhitaji wa Elimu hii pamojana Taulo za kike ni muhimu sana hususan ni sisi wanafunzi ambao Tunakaa katika Mabweni".
Alisema Aisha Muhammed Omar Mwanafunzi kidato cha Tano Skuli ya Sekondari Madungu Chake Chake Kusini Pemba.
"Kitendo hiki kilichofanywa na Bare foot in kwetu kitakuwa Faraja kubwa Kitasaidia kutupunguzia gharama za ununuaji wa Pedi na Sabuni na pesa zitatusaidia kutumia matumizi mengine ya muhimu tukiwa hapa Skuli" Alisema Nassra Andalla Omar Mwanafunzi.
Aidha kupitia Siku hiyo Wanafunzi hao pia wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba kuwasaidia Kupata huduma Ya Maji ya uhakika Katika Skuli yao, Dampo la kutupa Taka, ili kuweza kuzidisha kuimarisha Matundu ya Vyoo ili kudhibiti kutopata Magonjwa ikiwemo UTI, pamoja naMagonjwa ya ngozi kwa wanafunzi wakike ambao wanakaa katika Madahalia
" Skuli yetu inaukosefu wa Huduma ya Maji hususan ni Sisi ambao tunakaa katika Dahalia hili la hapa Nje ya Skuli, Jambo ambalo linapelekea kutumia Maji kwa umakini kutokana na Upungufu huo hivyo, Usafi Unapungua, Maradhi yanajitokeza Wengine wameanza Kupata maradhi ya Ngozi, Vyoo havifanyiwi usafi wa kutosha tunahofia kupata maradhi Ya UTI, Walisema Asma Ameir Khamis, Awena Khamis Ali, Pamoja na Faidhat Adam Kombo baadhi ya wanafunzi wanaosoma na kukaa katika Dahalia Skulini Hapo.
Awali akitoa Elimu Juu ya Mfumo wa Afya ya Uzazi wa Mwanamke Daktari Mstaafu Kutoka Hospitali ya Wilaya Chake Chake Mwajuma Ali Shehe Aliwataka Wanafunzi hao Kujiepusha na vishawishi ili kuepuka Athari ambazo zinaweza Kujitokeza kutokana na Maumbile yao .
Mfumo wa uzazi wa mwanamke Ni rahisi sana inapotokea Mtoto wakike kavunja ungo kupata Matatizo ikiwemo ujauzito hivyo niwasihi wanafunzi msije mkajaribu Mambo ambayo licha ya kuwa Maumbile Yenu ya Mfumo wa uzazi yamewaruhusu lakini Kwa Umri wenu ni Athari kubwa Mzingatie, Kusoma na Endapo mtaona dalili ambazo ni Tofaui Msisitekuwashirikisha wazazi wenu kwajili ya Usalama Zaidi".
Akizungumza Mkurugenzi Miradi kutoka Taasisi ya Barefoot College International Zanzibar Brenda Geofrey, Amesema kukabidhi Vifaa hivyo kwa Wanafunzi ni katika kuadhimisha siku Ya Hedhi Salama Duniani ambapo Taasisi hiyo kwa kuushirikiana na Dnata imedhamiria kuwafikia Jumla ya Wanafunzi 300 katika Skuli Nne Tofauti katika Maeneo mbali mbali ya Vijijini ambapo katika Skuli hiyo jumla ya Wanafunzi 70 wamekabidhiwa Vifaa hivyo kwajili matumizi salama wanapokuwa katikKipindi Cha Hedhi .
Mwisho.
Comments
Post a Comment