CP ZANZIBAR AFUNGA MAFUNZO YA SAJENTI (SGT)NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR
Na Omar Hassan Unguja
KAMISHNA wa Polisi Zanzibar CP Hamad Khamis Hamad amefunga mafunzo ya uongozi mdogo ngazi ya Sajenti na kuwataka Askari waliomaliza mafunzo hayo kufanya kazi kwa uwadilifu na haki wanapotoa huduma kwa wananchi.
Akifunga kozi nambari 1/2023 ya cheo hicho cha SGT huko Chuo cha Polisi Ziwani CP Hamad alisema mafunzo hayo yatakuwa kichocheo cha kuendeleza nidhamu, weledi, haki na uwadilifu.
Aidha amewahimiza wahitimu hao kutumia mafunzo waliyoyapata kulisaidia jeshi na wananchi katika kukabiliana na uhalifu na wahalifu.
Comments
Post a Comment