MWAKILISHI VITI MAALUM KUSINI PEMBA NEEMA KWA AKINA MAMA WAJASIRIAMALI.
Na Amina Ahmed Moh’d Pemba
Mwakilishi wa Viti Maalum kupitia Jumuiya ya Wanawake(UWT) Mkoa wa Kusini Pemba Leila Muhammed Mussa amekabidhi vyerahani 8 kwa wanawake na wanavikundi vya UWT Mkoa huo na vifaa vya ujenzi ikiwemo Bati 80 na Matufali 500 kwa ajili ya ujenzi wa maskani na ofisi Pamoja na Fedha .
Akikabidhi vifaa hivyo huko Baraza la Mji Chake Chake Leila amesema lengo la kukabifhi vyerahani hivyo kwa wanavikundi vya UWT ni kutaleta ukombozi wa Kimaendeleo kwa akina mama katika kujikwamua kiuchumi.
Alisema kuwa vifaa vya ujenzi Vitasaidia kukamikishia na kuendeleza ujenzi wa Maskani na matawi ya chama kwenye yaliopo katika Maeneo mbali mbali Mkoa huo.
Alisema wao kama viongozi walipata dhamana ya kuwawakilisha wanawake kupitia Jumuiya kwenye vyombo vya kutunga sheria na serikalini wanao wajibu wa kujengea uwezo wanachama wao waweze kujikwamua na umaskini.
Aidha Waziri Leala aliwahimizwa wanavikundi waliopatiwa vyerahani hivyo kuvitumia ili waweze kuongeza kipato chao.
“Sisi kama viongozi muliotuamini kutupa nafasi hii hatuna budi kuwawezesha wanawake wana CCM wenzetu na vikundi vya UWT ili kujikwamua, nafamu charahani hizo ukishoni kitenge, kanzu mutapata chochote kiweze kuwasaidia”
Kwa upande wake Katibu wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba Asila Ali Salim amempongeza Mwakilishi huyo ambaye pia ni Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kwa kutoa vifaa hivyo.
Alisema moyo ulioonyeshwa na mwakilishi huyo ni mfano wa kuigwa na wengine kwa kusaidia chama na wanachama wenzao nila ya kujali ni eneo gani alilotokea .
Naye Mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Kusini Pemba Zuwena Abdalla Haji alimpongeza Mwakilishi huyo wa viti maalum kwa kutekeleza kwa vitendo ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM kwa kujali ahadi alizowaahidi wanachama na wananchi kwa ujumla kwani hiyo ndiyo ccm.
Naye Asha Kombo Yussuf kutoka UWT Tawi la Wawi ametoa shukurani zake za dhati kwa Mwakilishi wao wa Viti Maalum Leila kwa kuwapatia msaada huyo kwani umelenga na kudhingatia kutatua changamoto za wanachama hao.
Naye akizungumza kwa niaba ya wanachama wa CCM Shehia ya Kilindi Sheha wa Shehia hiyo alimuahidi Waziri Leila kuwa atahakikisha vifaa vya ujenzi walivyokabidhiwa kwenye shehia yao vinatumika kwa vile ilivyokusudiwa.
Pia Mwakilishi huyo alikabidhi bati kwa wanawake wa UWT Wilaya ya Micheweni Pemba na kueleza kuwa yeye ni kiongozi anayetokanana CCM hivyo popote atakapoombwa kusaidia hatasita hata ikiwa sio mkoa wake anaotoka.
Mwisho
Comments
Post a Comment