UELEWA WA KURIPOTI MATUKIO YA UDHALILISHAJI WA KIJINISIA KATIKA JAMII UMEONGEZEKA, WANAMTANDAO WAPEWA MASHIRIKIANO NI BAADA YA KUANDALIWA NA TAMWA-ZANZIBAR KUIFIKIA JAMII.
Na Amina Ahmed Moh’d, Pemba ( 0719859184).
UELEWA katika Kuripoti Matukio mbali mbali ya Udhalilishaji wakijinsia kwa wanawake na watoto yanapojitokeza katika Jamii kisiwani Pemba Imeelezwa kuongezeka baada ya wanachi kuendelea kutoa mashirikiano kwa wanamtandao pamoja na kutumiaJukwaa la Habari kuripoti Matendo hayo yanapojitokeza.
Hayo yameelezwa na Wanamtandao wa kupinga udhalilishaji wa Kijinsia Kisiwani Pemba katika Mkutano maalum wa kuwasilisha Ripoti ya Ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na Udhalilishaji walioifanya katika kipindi cha Miezi 5 kutoka maeneo mbali mbali ya shehia za Kusini na Kaskazini Pemba.
Wamesema awali Jamii ilikosa Imani juu ya Mtandao huo wa kufatilia Masuala hayo Lakini kwa sasa uelewa umeongezeka na wanaendelea kupata Mashirikiano katika kuendeleza mapambano hayo.
" Jamiii, Walikuwa wanaona kama sisi hatuna nia ya kupambana na Udhalilishaji, lakini kila siku zilivyozidi waliona juhudi zetu za kupambana na Vitendo hivyo za zati wamekuwa mstari wa mbele kutuunga Mkonona kututafuta kila inapotokea au kuskia kesi hizo wanatutafuta"
Tunashukuru Kupitia Mashirikiano ya wananchi Tumeweza kutatua kwa pamoja changamoto mbali mbali za Udhalilishaji ambazo zilikuwa sugu Kama kutorosha,na Wahalifu kukimbizwa baada ya Kufanya matukio. Alisema Bakar Khamis Khalid Wanamtandao huo Kutoka Wilaya ya Wete.
" Waalimu wa Madrasa Tulikuwa Tunapata ugumu wa kuwafikia Lakini Tumekuwanao karibu na wao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa Mashirikiano kwa Waalimu wa Madrasa wengine katika kutoa elimu na kuendeleza Mapambano haya" Alisema Ustadh Juma Said Mwanamtandao kutoka Kengeja Wilaya ya Mkoani.
kwa upande mwengine Wanamtandao hao pia wameiomba Taasisi ya TAMWA-Zanzibar, pamoja na Serikali Kuendelea kuwasaidia kasi ya kuripoti Matukio ya ulawiti unaoendelea kufanywa na watoto wenyewe maskulini, sambamba na kuwezesha kuundwa kambi maalum katika shehia Ambazo zitasaidia kujenga uelewa kwa Watoto wanaofanya vitendo hivyo kwa kujielewa.
"Wimbi la watoto zaidi ya 20 wamekuwa Wakifanya mchezo huu wa kulawitiana wenyewe kwa wenyewe, Na wimbi hili nimelibaini Katika Shehia yangu Ya kiwani nilipopita Kutoa elimu kwa wanafunzi, Tunaomba Mtusaidie kuliangalia suala hili na Shehia nyengine Ili kushibiti Mtino huu kwa wanafunzi Wadogo, wenyewe kwa wenyewe ambao wamefundishwa mtindo huu mchafu na Mtu mzima Anaejielewa Alisema Mwanaidi Vuale Khatib.
"Kamati maalum, pamoja na Maeneo maalum ambayo yatasaidia kubadili Tabia kwa watoto watukutu ambao wamekuwa wakifanya vitendo hivi kwa watoto wenzao, Serikali Pamoja na Tamwa Zisaidie kuwepo kama sio katika kila shehia bhasi Angalau katika wilaya ili kuona tabia kwa watoto waaina kama hizi zinabadilika. Awena Salum kombo Mwanamtandao Kutoka Kangagani.
Aidha wameiomba chama hicho Kuzidisha kutoa Elimu kwa Waalimu wa Madrsa ambao wamekuwa wakiona ugumu kuzungumzia Masuala haya ya Udhalilishaji kutokana na Sababu zao binafsi na kushindwa kutoa Mashirikiano wanapofikiwa na Wanamtandao huo.
Kw upande wake Mratibu wa TAMWA-Zanzibar ofisii ya Pemba Fat-hiya Mussa Said amewataka wanamtndao hao wa Kutumia Jukwaa la Habari kumaliza Udhalilishaji kuzidisha kasi ya Ufuataliaji wa Matukio hayo yanapojitokeza katika jamii ili kuzidha kasi ya mafanikio katika kuibua changamoto za udhalilishaji Ili ziweze kumalizika.
"Wanamtandao Mnafanya kazi kubwa Sana Kasi hii isiwe tu baada ya kumalizika kwa mradi bali iwe endelevu hata baada ya kumalizika Meadi huu tunataka kuona Mabadiliko zaidi katika kuibua kuriooti na kuchukuliwa hatua Kesi mbali mbali za Udhalilishaji Zinapotokea katika Shehia Zetu.
Mkutano Huo wa Siki Moja wa kuwasilisha Ripoti ya ufuatiliaji wa Matukio ya Udhalilishaji kwa Wanamtandao ni katika utekelezaji wa Mradi wa Tumia Jukwaa la Haari Kumaliza Udhalilishaji unaotekelezwa na Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar pamoja na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Nchini Denmark (DANIDA).
Mwisho.
Comments
Post a Comment