VITENDO VYA UDHALILISHAJI VINAVYOFANYWA KWA SIRI NA WANAFAMILIAKUIBULIWA NA USALAMA WETU KWANZA



NA OMAR HASSAN – ZANZIBAR                                                

Mkuu wa Intelijensia ya Jinai Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Kombo Khamis Kombo amesema walimu wa usalama wetu wanaosomesha skuli za msingi wanaibua kesi za udhalilishaji wa watoto ambazo huwa haziripotiwi vituo vya Polisi kutokana na muhali wa wanafamilia.

Akifunga mafunzo ya Usalama wetu kwanza huko Chuo cha Polisi Zanzibar amesema masomo hayo yanawafanya wanafunzi kujitambua na kuwapa ujasiri, hivyo huwa wanatoa taarifa kwa walimu Polisi endapo wamefanyiwa udhalilishaji ambapo mwaka 2022 Matukio 57 waliyaripoti wanafunzi ambayo yanaendelea kufanyiwa kazi katika Vyombo vya sheria.

Mkuu wa Polisi Jamii Zanzibar, Kamishna Msaidizi wa Polisi Dkt. Egyne Emmanuel amesema Jeshi la Polisi limeanza kutoa elimu katika ngazi za awali kutokana na wahalifu walio wengi hujifunza uhalifu wakiwa katika umri mdogo.

Aidha Mratibu wa Program ya Malezi mbadala ya kijamii Shirika la SOS Nyezuma Simai Issa amesema Jeshi la Polisi kusimamia ulinzi na usalalama wa maisha ya watu na mali zao kwa kutoa elimu kwa watoto ni jambo la msingi.

Nae Afisa kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Anina Salum Khalfan amesema kutokana na umuhimu wa somo la Usalama wetu Kwanza, somo hilo watalifundia pia katika Madrasa.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI