Jee ni kwa namna gani yataweza kufikiwa Maendeleo ya Elimu ambayo itakuja kuwa mkombozi baadae katika maisha ya mtoto wa kike ni pamoja na kuwa na Afya imara mazingira salama na upatikanaji wa huduma muhimu ambazo zitasaidia kuondosha usumbufu wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi.
Wanafunzi wengi wakike ambao wamefikia umri wa baleghe ( kuvunja ungo) wakiwa katika harakati za kutafuta Elimu.
Wapo wanaolazimika kukaa katika madahalia ili kuona ndoto ya kupata elimu bila usumbufu ,lakini pia wapo ambao hulazimika kuwekewa mazingira maalum ambayo yatawarahisishia upatikanaji wa Elimu kwa kukaa katika nyumba maalum kujisomea.
Huduma Muhimu ambazo zinaulazima katika kufikia afya bora ya Mwanafunzi wa kike ni pamoja na Kuwepo na mazingira rafiki ya kutumia wanapokuwa katika kipindi hicho cha Hedhi.
Changamoto hizo ndizo ambazo zimenifanya niandae Makala hii maalum ambayo itasaidia kukumbusha serikali wizara ya Elimu pamoja na wadau wa maendeleo ya mwanafunzi wa kike kuhusu kadhia hizi ambazo endapo hazitoangaliwa kwa jicho la tatu huenda hedhi salama ikaendelea kubaki kwa maneno bila uhalisia kwa wanafunzi wa kike.
Mazingira hayo ni pamoja Huduma ya maji safi vyoo salama, ,elimu kuhusu afya ya viungo vya uzazi kwa mwanamke,vyumba vya kujisitiri na kuvaa nguo, kupatikana kwa Taulo za kike kwa wakati mazingira maalum ya kutupia Taka (Jaa).
" Skuli yetu inaukosefu wa Huduma ya Maji hususan ni Sisi ambao tunakaa katika Dahalia hili la hapa Nje ya Skuli, Jambo ambalo linapelekea kutumia Maji kwa umakini kutokana na Upungufu huo hivyo, Usafi Unapungua, Maradhi yanajitokeza Wengine wameanza Kupata Maradhi ya Ngozi, Vyoo havifanyiwi Usafi wa kutosha tunahofia kupata Maradhi Ya UTI, Ni maneno ya Mwanafunzi Asma Ameir Khamis, Awena Khamis Ali, Pamoja na Faidhat Adam Kombo baadhi ya wanafunzi wanaosoma na kukaa katika Dahalia Skuli ya Sekondari Madungu Chake Chake.
"Ni Afadhali Wanaotoa misaada Watupigie Kelele Kupata Maji Ya kutosha katika Skuli yetu Kwa sababu Nasubutu kusema kuwa Kipindi Cha Hedhi kwetu bila maji ya kutosha ni Uchafu Zaidi Vyooni, jambo ambalo ni Athari kwa afya Zetu sisi watoto" Aisha Omar Abdalla Mwanafunzi kidato cha Tano Madungu Sekondari.
"Hatuna Dampo Skulini kwetu tunalazimika Kuweka Pale katika Madude ya kuhifadhia Taka Ili Watu wa Usafi wa Baraza waje kuchukua Siku nyengine inafika Siku tatu hawajaja Uchafu Unakaliana Tunaiomba Serikali Kuliangalia Suala Hili".
Baadhi Wanafunzi wa kike wanatumia Matambara wakati wa Hedhi kutokana na kutoweza kumudu Bei Ya Taulo Baadhi ya Wanafunzi Huku wengine Tukiona kama ni Ugonjwa Ambao kwa Tamaduni zetu kumueleza Baba au mama Tunaisikia Aibu sana, kwa kweli, inaskitisha mno kwani Matambara hayo yanaweza kuacha Madoa ya hedhi kwenye nguo zetu za Skuli Pamoja na nguo za ndani". Alidai Fatma Abdalla Mbarouk Kutoka skuli ya Sekondari Msuka.
" Wahisani Waliangalie na Suala la Maji katika skuli yetu ya Msuka Sekondari Wanafunzi wa kike Tunapitia changamoto Kipindi cha Hedhi, na naamini sio Skuli yetu peke na yengine pia" Ruwaida Salum Hamad Mwanafunzi Msuka Sekondari Wilaya ya Micheweni.
" Bado Tunadhana potofu juu ya Suala la Hedhi binafsi Sijawahi kuumwa na Tumbo la hedhi nikamwambia Mzazi wangu wa kiume Na hata mama naona ugumu sana hulazimika kuja Skuli na Maumivu yangu nikifika Siwezi kusoma wala sikai kwa utulivu ila inanibidi nikae hivyo Tunaiomba Serikali iweke suala hili la Afya ya uzazi kuanzia madarasa ya nne ambapo wanawake wengi huanza kupata baleghe" Thuwaiba Juma Muhammed Skuli ya Sekondari Chambani Kusini Pemba.
"Mimi naona Ninapokuwa katika siku zangu Kwanza nakuwa kama nina maradhi ya kuenda Chooni mara kwa mara, Huku naona kama nadhuriwa na vyakula na maji kwa sababu nakuwa nafanya kama ugonjwa wa ngozi mwilini kila ninavyitumia Maji naona hayatoshi Nakuwa na wasi wasi mkubwa na Mazingira Ya kutupa Pedi Nahofia Sababu Vyoo ni vichache Ukilinganisha na wanafunzi Tuliopo hapa Pindua tupo kuanzia Kidato cha Kwanza "Zubeida Amour Skuli ya Sekondari Muhammed Juma Pindua.
Nasubutu kusema wazazi Sijui tumewalea kwa kutokiwa wawazi watito wetu wakike Lakini Hili suala kwao wamekuwa kama ni aibu au siri ambayo wanahisi mzazi hastahiki kujua hususan ni sisi Akina baba, Binafsi mimi nina watito wakike wakubwa lakini kama sio mama yao kuniambia wao hawajawahi kuniambia masuala hayo kabisa , Wito wangu Tubadilike Alisema Muhammed Salum Mzazi Madungu.
Ofisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba Muhammed Nassor Salum amesema kuwa licha ya jitihada za Serikali na wadau bado tatizo la Hedhi Salama Skulini linahitaji Mikakati Endelevu, kutokana na Umuhimu wake .
"Wizara ya Elimu inafanya Jitihada mbalimbali ikiwemo kuimarisha Miundo mbinu kuwa Rafiki kwa watoto wakike, Kutumia vyumba maalum wanapokuwa katika Vipindi vya Hedhi, waalimu washauri , Taulo zinakuwepo Mashuleni Maji lakini bado inakuwa havijitoshelezi kwa vile suala hili ni endelevu kwaio Tunaendelea na namna bora ya kuliangalia suala hili katika mikakati endelevu Ili kuona watoto wakike hawakosi masomo wanapokuwa katika Mzunguko.
Kwa Mujibu Waziri wa Afya Tanzania Ummi Mwalim Asilimia 48 ya wanafunzi wa kike wanakosa Masomo kutokana na kuwa katika mzunguko wa Hedhi hali ambayo huathiri uwezo wa wanafunzi hao kujifunza kwa ufasaha.
Takwimu zilizofanywa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu kwa kushirikiana na Maabara ya Afya ya Jamii Pemba uliowafikia wanafunzi wakike kwa Asilimia 78 katika mahojiano ndani ya Skuli 294 Katika Mikoa 19 Tanzania Bara na Zanzibar ambapo utafiti huo Ulionesha kuwa Asilimia 48, ya Wanafunzi Waliohojiwa walisema kuwa huathirika na kupoteza uwezo wao wa kujifunza kutokana na Sababu mbali mbali ikiwemo Maumivu ya Tumbo , Kukosa Taulo, Maji na Mazingira rafiki wanapokuwa Skuli.
Ikumbukwe kuwa kampeni ya Taifa ya Usafi wa Mazingira kupitia Mpango Endelevu ya Maji na Usafi wa Mazingira Skuli na vijijini Mwaka 2020/21, ilieleza kuwa Serikali ya Tanzania imeweza kujenga Miundo mbinu ya vyoo vikiwemo vya Wanafunzi wenye ulemavu pamoja na sehemu ya Hedhi salama ambayo ina vifaa muhimu vinavyohitajika katika shule 835 kwenye Mikoa 17 pekee.
Aidha Kwa Mujibu wa Taarifa iliyitolewa na Ofisi ya Takwim Tanzania (NBS) juu ya masuala ya Maji na usafi Mazingira skulini mwaka 2018 inaonesha asilimia 66.8 ya shule ndizo zina huduma ya Hedhi salama ambapo kati ya hizo zilizobainika kuwa na viteketezi ni asilimia 24 huku asilimia 22.8 zinatupa taka kwenye mashimo na 19.5 zina vichomea Taka visivyokidhi.
Hata Hivyo kwa Visiwa vya Unguja na Pemba Serikali Ya Mapinduzi kupitia Wizara ya Afya Kitengo Cha Lishe Kilifanya Utafiti Mdogo Mwaka 2022 karika skuli mbali mbali Na kubaini kuwa Asilimia 25 ya Mahudhurio ya Skuli kwa Wasichana wakati Hedhi, hawahudhurii ioasavyo, huku Ikibainisha kuwa Asilimia 12.5 wakihudhuruia bila kuwa na Usomaji mzuri kutokana na sababu mbali mbali za Kiafya.
Comments
Post a Comment