WANANCHI WAMPONGEZA KADUARA UTENDAJI WAKE JIMBONI WAAMUA KUMUITA TENA KUONGEZA KASI YA UJENZI WA MAENDELEO.
Na Amina Ahmed Moh’d Pemba (0719859184).
WAKAAZI wa Kijiji cha Madungu Kosovo Wilaya ya Chake Chake Wamemuomba Mwakilishi wa jimbo hilo Shaibu Hassan Kaduara Kuendeleza Ujenzi wa Barabara aliyoanza kuijenga Na kuwa Faraja kwa wakazi wa kijiji hicho katika kurahisisha huduma zao mbali mbali, jambo ambalo awali halikuweza kufanywa na viongozi waliopita ndani ya jimbo hilo.
Wakizungumza baadhi ya Wakaazi hao wamesema Ujenzi wa barabara hiyo ulioasisiwa na Mwakilishi wao wa jimbo la chake chake umesimama kwa Muda huku kifusi kilichowekwa Awali kikianza kuburutwa na Maji baadhi ya Maeneo ya barabara hiyo kutokana na kusita kwa Ujenzi huo.
Wamesema Matumaini yao ni kukamilishwa kwa kiwango cha lami Barabara hiyo ambayo licha ya kuwahaijakamlika lakini inaendelea kuwa faraja kwawananchi wa kjiji hicho hado sasa.
"Mwakilishi wetu Amefanya jambo kubwa ambalo hatukuwahi kulitegemea , lakini yeye ameweza katuahidi kutuletea Barabara kijijini kwetu na kafanya hivyo na mengi Mazuri Tunampongeza sana, Furaha yetu ni kuona inakamlika kwa kiwango cha Lami Barabara hii haiishii hapa ilipofika, tunamuomba Mwakilishi Wetu azidi kuifanyia Maboresho ili ikamilike kwa kiwango cha lami na iweze kudumu kwa muda mrefu,"Alisema Hamadi Mbarouk mkaazi wa Kosovo Madungu.
" Kwetu wakaazi wa Kosovo Kaduara kawa Mkombozi Wawakilishi waliopita walikuwa hawajui kama kuna kijiji kabisa ambacho kinahitaji barabara lakini yeye tumekuwa tunamuona mara kwa mara anakuja Tunamweleza Changamoto zetu mbalo mbali tunaamini atakaposikia taarifa hizi ataipa uzito jambo hili.
, Gari zilikuwa hazijui zinafika wapi wagonjwa tulikuwa tunalazimika kuwabeba kwa vitanda mpka kufika kwenye barabara mbali na kijiji Chetu, Harusi misiba, mizigo harakati za vifaa vya ujenzi lazima tulikuwa tunasumbuka lakini saivi Baada ya kuchongewa baranara tunaendesha shuvhuli hizo bila usumbufu.
"Tunaamini Majukumu Mazito ya Kiutendaji ndiyo ambayo yamemfanya ashindwe kuiendeleza hii barabara kwa hatua zilizobakia, na imani yetu atakapomaiza hayo majukumu atarudi kuliangalia hili ambalo hata yeye ni moja kati ya vitu vya kujivunia.
Kiukweli tumeondokana na usumbufu katika harakati zetu baada ya kupata hii njia, hatua hii imeanza kutupa matumaini ya kupatikananjia ya kuingia na kutoka kijijini humo ambayo inatusaidia tunaitumia katika harakati mbali mbali bila usumbufu.
Miaka mingi imepita kijijini kwetu hakuna barabara ya uhakika wala hatukuwa na matumaini kama kuna siku tutaweza kupata ufumbuzi wa suala hili lakini kwa sasa tunamatumaini makubwa kuweza kupata njia.
Alisema Asha khamis Idi mkaazi wa Madungu Kossovo Hapa ilipofikia tumeanza kuitumia.
Ombi hilo limekuja baada ya wananchi wa kijiji hicho kuonekana katika harakati za Kujaza mchanga katika moja ya njia hiyo iliyoanza ujenzi wake na Mwakilishi wa Jimbo la Chake Chake Shaib Hassan kaduara na kuonekana ikiwa tayari imeanza kuchimbuka huku ujenzi ukiwa umesimama kwa Takriban miezi Mitano Sasa.
Harakati za kumtafuta Mwakilishi wa Jimbo hilo kulizungumzia Suala hili zinaendelea.
Comments
Post a Comment