ZSSF PEMBA YATOA TAHADHARI KWA WASTAAFU , NI BAADA TA KUJITOKEZA MATAPELI KUTUMIA VIBAYA KAULI YA DK MWINYI KUONGEZA PENCHENI KUIINUA MGONGO.
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA (0719859184).
UONGOZI wa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar Zssf Pemba Umewataka Masheha Kutoa Taarifa za uhalifu na Utapeli zinazoendelea Kujitokeza katika Shehia zao Ambazo zinafanywa na baadhi ya watu ambao sio waaminifu kwa kutumia jina na mwamvuli wa mfuko huo na kufanya udanaganyifu kwa wazee wastaafu wakidai kuwa wanafanya usajili kwajili ya kupata Pencheni zao kwa haraka na kuwachukulia fedha .
Akizungumza na Waandishi wa Habari Kaimu Mkurugenzi Zssf Pemba Dk. Said Salim Maalim Amesema watu hao ambao wamekuwa wakipita katika maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba wakiwaeleza wazee wastaafu kuwa wao ni Wafanya kazi kutoka Hazina Zssf na kujitambulisha katika Uongozi wa Shehia Na hatimae kupata ruhusa ya kuingia Mitaani kufanya udanganyifu huo limekuwa likijitokeza katika maeneo mbali mbali hivyo Masheha kuendelea Kuchukua Tahadhari ili wazee na wastaafu wasiendelee kutapeliwa.
" Matukio haya ya Udanganyifu yameanza kujitokeza takriban Shehia Nne wilaya zote za Pemba na Watu hawa ambao wanafika katika uongozi wa Shehia kujitambulisha na kuingia katika majumba kufanya udanganyifu huo, Tuweke wazi kwamba Zssf haiwatambui hivyo Wananchi endeleeni kuchukua Tahadahri, kuepuka utapeli huu.
"Hawa ni watu ambao hawapendi Maendeleo na wanaitumia vibaya kauli ya Mh Rais Wa Zanzibar Aliyoitoa Siku ya Wafanya kazi juu ya kuongeza Pencheni (Kiinua Mgongo) kwa Wastaafu kwa kuwafuatamajumbani kuwarubuni na kujipatia wao kipato kwa njia ya udanganyifu kwa kutumia mwemvuli wa mfuko wa Zssf jambo ambalo ni kinyume na Sheria.
Aidha Kaimu Mkurugenzi huyo amesema tayari Uongozi wa Zssf Pemba umeanza kulichukulia hatua Suala hilo ikiwa ni Pamoja na kuweka taarifa katika Vyombo vya Ulinzi na usalama Jeshi la Polisi.
Hata hivyo Amewataka wastaafu wote wanaopokelea pencheni Zao Katika Mfuko Huo kuendelea kufuata utaratibu waliowekewa na Zssf ili kuepusha Usumbufu huo.
" Kupitia vyombo vya habari niwasihi wastaafu muache kuamini i maneno yanayotolewa mitaani kutoka kwa watu watu wasiokuwa na nia njema na Serikali,Zssf ipo Na itakapobadilisha utaratibu juu ya Jambo lolote mtajuilishwa kwa utaratibu maalum msikubali utapeli, kwa Mabadiliko ya nyongeza za Pencheni mkarubuniwa jambo ambalo liliwekewa utaratubu maalum kwa wastaafu wote
Kwa Upande de wake Raya Hamdan Khamis Ambaye ni Afisa uhusiano na Elimu kwa Umma ( Zssf ) Pemba amewataka Masheha Kutowaamini wau ambao wataingia katika shehia Bila utambulisho maalum ikiwemo barua Rasi kutoka taasisi husika ili kuepusha kadhia kama hizo kwa wazee.
Udanganyifu huo ulioripotiwa kutoka maeneo mbali mbali Pemba umeelezwa kuwa zaidi ya wastaafu 4 wamefanyiwa udanganyufu huo na kurubuniwa shilingi elfu 80 kila mmoja, katika wilayaya wete, Shehia ya Jadida, Gando, Mkoani, pamoja na Chake Chake.
Mwisho.
Comments
Post a Comment