WAHANDISI KUKAMILISHA MIRADI KWA WAKATI
NA HASSAN MSELLEM PEMBA.
Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA, Balozi mstaafu na Meja Jenerali Issa Suleiman Nassor, amewataka wahandisi wa miradi ya maji Kisiwani Pemba kuhakikisha wanakamilisha miradi hiyo kwa wakati.
Ametoa kauli hiyo huko katika Mradi wa tangu la maji Shumbamjini katika ziara ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maji Kisiwani Pemba kupitia fedha za ahuweni za Uviko19, amesema azma ya Serikali ni kuhakikisha miradi hiyo inakamilika ifikapo Mwezi Julai mwaka huu ili wananchi waondokane na changamoto ya ukosefu wa huduma ya maji safi na salama inayowakabili.
Kwa upande wake mjumbe wa bodi ya Wakurugenzi wa Maji Zanzibar ZAWA, Mheshimiwa Mohammed Aboud Mohammed, amewataka wananchi Kisiwani humo kuvitunza vyanzo vya maji ili huduma hiyo iweze kupatikana kwa urahisi.
Nae Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar ZAWA Kisiwani Pemba, Bakari Mshindo, amesema kupitia miradi hiyo ya fadha za Uviko19 wamefanikiwa kuchimba visima 27 pamoja matangi matano ya kisasa katika Wilaya zote za Pemba.
Ziara hiyo ya siku mbili ya Wakurugenzi wa bodi ya Mamlaka ya Maji Zanzibar Kwa kushirikiana na watendaji wa Mamlaka ya Maji Kisiwani Pemba wametembelea miradi mbali mbali ya maji Kisiwani Pemba.
Comments
Post a Comment