KONDE WAMPONGEZA MWAKILISHI ZAWADI KUWASAIDIA KUPATA HUDUMA ZA KIJAMII.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA.
BAADHI ya Wananchi na wakaazi wa Konde Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba wamesema kasi ya Maendeleo inayoendelea kuoneshwa na Mwakilishi wa Jimbo hilo Zawadi Amour Nassor katika nyanja mbali mbali Ikiwemo Maendeleo ya Elimu pamoja na Upatikanaji wa Huduma ya safi na Salama imekuwa ikisaidia kuondosha Usumbufu waliokuwa wakipata Awali wao pamoja na watoto.
Wakizungumza na Habari Hizi Halima Juma Khamis Mkaazi Wa Matangatuani Konde Mkoa Wa Kaskazini Pemba Pamoja Na Nunu Khamis Mkaazi wa Kiuyu kwa Manda Wamesema Usumbufu waliokuwa Wanapata Wanafunzi wa Kijiji hicho kufata Elimu masafa ya mbali ulikuwa ukiathiri kwa kiasi kikubwa Maendeleo yao.
"Tunashukuru Mwakilishi wetu wa Jimbo la Konde Mh Zawadi kwa kutusaidia kupatikana Skuli mbili Maeneo ya karibu ambazo zimeondosha usumbufu kwa watoto wetu, Walikuwa wanalazimika kuenda Mgogoni jambo ambalo lilikuwa ni usmbufu kwao" Alisema Bi Nunu.
" Hapakuwa na Skuli hapa zamani Kila siku tulikiwa tunatoa malalamiko yetu Tulipopata Kiongozi anaejuwa Machungu ya Kufuata mbali Elimu Tunashukuru Ameisogeza huduma hii karibu Leo kijijini petu zimejengwa Skuli Mbili ambazo watoto wetu wanasoma Matangatuani na Kule Meli 9 Tunashukuru sasa wanafunzi hawaendi tena mbali Mgogoni au Konde wanasoma hapa hapa".Alisema
Watoto wetu wadogo miaka 4 mitano walikuwa hatarini kutokana na kukosekana Skuli apa kiuyu kwa Manda Walikuwa wanatembea umabli mrefu kukatisha mabarabara, Huku roho zilkuwa hatarini hofu ya udhalilishaji tulikuwa tunalazimika kuvunja shughuli zetu kuwapeleka Lakini leo Adha imepungua Alidai Bi Nunu.
Kwa upande wao Baadhi ya vijana wa jimbo hilo ambao wanaendesha Boda boda kujipatia kioato Wamemshukuru Mwakilishi Zawadi kwa kuwasaidia kupata Elimu juu ya Usalama Wa Barabarani.
Nilikuwa naendesha tu kienyeji enyeji sijasoma lolote Mwakilishi wetu Alifanikisha Mimi na wenzangu wengi ambao tunafanya kazi hii kusoma Tulitoka hapa konde Hadi micheweni kupata Mafunzo ya udereva na leo hii yanatusaidia kudhibiti ajali za kiholela Tunamshukuru kwa mchango wake. Alisema Said Suleiman.
Wakizunguzia Suala La Maji Baadhi ya Wananchi Wa Jimbo hilo walisema kuwa usumbufu waliokuwa wanaupata awali kutafuta huduma ya Maji umeondoka kutokana na Kujengewa Visima ambavyo Vinasaidia Kupatikana Maji kwa urahisi.
Akizungumza na Habari Hizi Mwakilishi Wa Jimbo Hilo Zawadi Amour Nassor Amesema Maendeleo hayo Ambayo Yanaendelea Kupatikana ndani ya Jimbo la Konde ni kutokana na Usimamizi mzuri wa Matumizi ya fedha za Mfuko Wa jimbo na Ushirikiano kutoka kwa Mashirika Mbali mbali.
" Niliahidi wakati Naomba ridhaa kwa Wananchi kupigania Maendeleo ya jimbo la Konde , kusimamia upatikanaji wa Maji ili kuwatua ndoo Kichwani akina Mama, ni kweli kwa Kushirikianana Direct aid Nimefanikiwa kujenga na kuchimba Visima 5 maeneo mbali mbali vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi Milioni 95,
Aliendelea kuwa "Na kupitia Maji ya Zawa nimefanikiwa kufikisha Maji ya bomba katika shehia ya Kifundi ambayo imekuwa ikipeleka maji hayo na sheia jiarani.
Aidha Alisema Mradi unaotekelezwa na Serikali juu ya Ujenzi wa Tangi la Maji Kipange unadhamira njema ya kuondoa usumbufu kwa wananchi wa Maeneo mbali mbali ikiwemo Makangale.
Mwakilishi huyo alisema kuwa Furaha yake kubwa ni kuendelea kutatia Shangamoto za wananchi ndani ya jimbo hilo na kuona wanaendelea kufurahia kupata huduma bora.
Mwisho.
Comments
Post a Comment