FURSA NA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI VIJANA KATIKA KUFIKIA MAENDELEO YA KUJIKOMBOA KIUCHUMI WAOMBA SERIKALI KUENDELEA KUWASAIDIA KUZIPATIA UFUMBUZI ILI KUZIDISHA KASI YA KUZIFIKIA FURSA MBALI MBALI KATIKA SIASA UCHUMI NA UONGOZI .
NA - AMINA AHMED MOH’D -PEMBA. MAENDELEO ya Nchi nyingi Yametokana na nguvu kazi pamoja ma Utendaji kazi wa vijana . Kila Taifa linategemea Vijana kufikia Malengo mbali mbali ya kukuza Uchumi na kuleta Maendeleo. Fursa mbali mbali ambazo vijana wamekuwa wakizitumia ndio siri pekee ya Kufikia Malengo ya kulipeleka mbele Taifa. Moja kati ya Sifa za kufikia Fursa mbali mbali ikiwemo Maendeleo kwa Vijana ni kuwa Na Elimu ambayo itasaidia kuongeza ufanisi juu ya Lile lengo lililokusudiwa la kuacha utegemezi na kujiajiri wenyewe Kupitia Fursa Zilizomo Katika Sekta na nyanja Mbali mbali ikiwemo Uongozi, Uchumi, Na Siasa. KIJANA NI NANI! ‘ ’KIJANA ni mtu yeyote mwenye umri wa miaka 15 hadi miaka 35,’’ndivyo sera na sheria ya vijana Zanzibar inavyofafanua. Lakini kwa upande mwengine kijana ametafsiriwa kuwa ni mwanamke au mwanamme yeyote mwenye miaka katia ya 15 hadi 24...