MWANAMKE ALIEPANIA KUKUKUZA KIPAJI CHAKE KWAAJILI YA KUISAIDIA JAMII.
NA SALMA SHAALI - UNGUJA
REHEMA Ali Mzee maarufu kama Ranisha ni binti mwenye umri wa miaka ishirini na sita (26) mkaazi wa fuoni pangawe (Unguja), ambae ni mwanamke aliepania kukuza kipaji chake kwaajili ya kuisaidia jamii,ambapo anajishuhulisha na biashara ya utengenezaji wa keki za aina tofauti pamoja na mchanganyiko wa viungo mbali mbali (rosted spice) ambayo hutumika katika vyakula tofauti ikiwemo supu ya kuku,mchuzi,biriani na vyenginevyo.
Rehema aliaza kazi ya kutengeneza keki tangu alipokuwa mdogo na alikuwa hajapa darasa lolote linalohusiana na utengenezaji wa keki, Baada ya kujigundua Kuwa anakipaji akaona ni vyema kuitumia fursa hiyo ili aweze kujiletea maendeleo pamoja na kuisaidia jamii yake iondokane na tatizo la uhaba wa ajira.Rehema anasema,
”Baada ya kujigundua kuwa nina kipaji na napenda kutengeneza keki nikaona nibora niende kwa mwalimu ili anifunze kutengeneza kwa ustadi zaidi na nina imani kuwa kupitia biashara hii ninaweza kuisaidia yamii yangu kuondokana na tatizo la ukosefu ajira”.
Mwaka 2021 Rehema aliaza kwenda darasani nahuku akifanya biashara na alipopata miezi miwili 2 watu wengi wakaaza kuvutiwa na biashara yake kutokana na ubora wa bidhaa zake na kadri siku zinavyoenda anazidi kuwa maarufu na biashara yake inazidi kukuwa jambo ambalo humpa matumaini ya kufikia malengo yake.
Kwa mujibu wa utafiti wa mwandishi wa makala hii umethibitisha kuwa watu wengine walipenda zaidi namna anavyoonesha ukarimu pamoja na kuwajali wateja wake kwani bei zake zimekuwa tofauti na bei za wafanyabiashara wengine maana wengi wao huuza keki kwa shilingi elfu ishirini na tano (2,5000), elfu arubaini na tano(4,5000),elfu hamsini( 5,0000) na kadri mnunuzi anapotaka keki nzuri na kubwa zaidi pia bei nayo huzidi lakini yeye anauza kwa bei moja tu ambayo ni shilingi 3,5000 wala hajali dizaini au mapambo makubwa anayoyataka mnunuzi.
Inawezekana kuwa wapo watu wanaotengeneza mchanganyiko wa viungo vya maii huko majumbani mwao lakini hadi leo mwanamke huyu ndie mtu pekee Zanzibar anaefanya biashara ya mchanganyiko wa viungo vya maji (rosted spice) ambayo inadumu kwa muda mrefu kama ule mchanganyiko wa unga,
”kutengeneza mchanganyiko wa viungo tofauti yaani rosted spice nilijifunza kutoka kwa dada yangu, na nilipogundua kuwa watu wengi wamezoea kutumia viungo vya unga ndipo nilipoamua kufanya kitu cha tofauti na niliongeza ubunifu wangu nikatengeneza mchanganyiko wa viungo ambao ni wa maji na unaweza kudumu kwa muda mrefu kama ule wa unga”,Amesema Ranisha ambae ni mwanamke aliyepania kukuza kipaji chake kwaajili ya kuisaidia jamii.
“kwakua najua kuwa tuna hali tofauti za maisha niliona nivyema biashara hii niifanye kwa ujazo tofauti ili kila mtu anufaike kwa mfano kuna ujazo wa shilingi elfu tatu na mia tano 3,500,elfu saba 7000,na ujazo wa elfu kumi 10,000”,Ameongeza Ranisha
Kutokana na ubunifu na utofauti wa biashara zake umewafanya watu wengi kuvutiwa na biadhaa zake na kila siku wamekuwa ni watu wa kumpongeza na kumsifia kwa kufanya biashara zakipekee tofauti na ilivyozoeleka. Sharifa Idrisa amabe ni mnunuzi wa bidhaa zinazofanywa na Ranisha anasema
”Mwazo tulikuwa hatufahamiani na nilikutana nae mtandaoni anatangaza huduma nami nikavutiwa kujaribu, kuna siku nikahitaji kutengenezewa keki nikamwambia nakaniletea ndani ya mda, nilipoonja nikavutiwa nayo kwasabu niliona inatofauti na ilikuwa nzuri sana, kwaiyo hadi leo ndio nikihitaji nachukua kutoka kwake”.
NANI ALIMSAIDIA KUKUZA KIPAJI CHAKE
Awali hakukuwa na mtu yeyote aliemwambia kuhusu kukiendeleza kipaji chake lakini kwakua alikuwa na hamu ya kuona kipaji chake kinakuwa na aliona ndio njia itakayomsaida kujiinua kiuchumi aliamua kuzungumza na wazazi wake ili waweze kumsaidia ushauri kuhusiana na maono yake.
Ranisha anaeleza ”Niliamua kuzungumza na familia yangu ili wanisaidie maana bila ya ridhaa yao nisingeweza kufanya kitu chochote,lakini nashkuru waliniunga mkono na kunisaidia kutafuta mwalimu pamoja mahitaji ikiwemo ada,naweza kusema wao ndio sababu ya mimi kufika hapa nilipo hivi sasa kwani wamekuwa mstari wa mbele kunishauri vitu vya maendeleo katika kazi yangu”.
“Aliponiambia kuwa anataka kujifunza kutengeneza keki sikumkatalia,nilimpeleka akasome ili nione kama kweli anania au anasema tu lakini kweli niliona alikuwa nayo maana ilikuwa akirudi kusoma anafanya mazoezi nyumbni na anamtumia mwalimu wake,sihaba saivi ameweza kufanikiwa ingawa sio sana lakini alipofika si padogo na kazi yake inapendwa zaidi kutokana na ubunifu wake”,Anasema Hawa Mahamudu Mzee ambae ni dada wa Ranisha amabe alimlea tangu alipokuwa mdogo hadi leo.
Hata hivyo,ndugu zake nao walieleza namna wanavyopenda juhudi zinazofanywa na dada yao,ambapo Shamir Shaaban Yahya anaeleza”Nafurahi sana kuona kwamba dada yangu amepata kitu chengine cha kufanya kwasababu sasa hivi tunaambiwa ajira hamna lakini yeye ameweza kujiajiri mwenywe, na kiukweli anafanya keki nzuri sana kwasababu kila anekuja kununua anazisifia na kusema kuwa ni nzuri”,
”Namshauri tu asiache kazi hii na aiboreshe zaidi kwa kuongeza mtaji,kufungua duka lake la kuuzia keki pamoja na kujitangaza Zaidi ili aweze kuchukuliwa na makampuni mbalia mbali maana sasa hivi kuna migahawa mingi inafunguliwa”, Ameongeza Shamir
Vile vile,wakati anawataja watu waliomsaidia kukuza kipaji chake alisema kuwa marafiki zake wanamsaidia sana katika kuitangaza kazi yake,”marafiki zangu wananisaidia sana katika kukiendeleza kipaji change kwani kuna siku naamka najikuta nimepostiwa mitandaoni mfano whatsapp,Instagram na mengine kwaiyo wananifaa kwa kiasi kikubwa”,Anasema Rehema
“ Tangu nimemjua Ranisha ni miaka miwili 2 sasa lakini tumekuwa marafiki wa karibu sana tunashirikiana vizuri kwasababu kuna vitu vingi tunashauriana ila napenda kuwa nae kwasababu anafanya kazi sana na anajielewa, yeye anatengeneza sana keki na anavyotengeneza kila mtu anapenda kwani anatumia ubunifu wa hali ya juu”,Amesema Aisha Said Omar ambae ni rafiki wa Ranisha.
FAIDA GANI ANAZIPATA
Siku zote kufanya kitu kizuri na kikapendwa na watu wengi hutokana na ubora wake hiyo ni moja kati ya faida za kitu hicho ingawa zitakuwepo na nyengine tofauti.Rehema anaelez “kwakua biashara yangu bado ni changa faida ninazozipata zinanisaidi kwa mahitaji madogo madogo,nashukuru mungu tangu nimeaza biashara hii na naenda zangu safari zangu sidai hata nauli maana kuna mtu haondoki bila kuomba nauli,sidai vocha ,nikikiona kitu njiani nimekipenda nanunu kama sina uwezo kwa wakati huo najipa mda kidogo baada ya wiki au mwezi pesa yangu imetimia naenda nanunua nihivo vitu ambavyo naweza kujikimu mimi kama mimi mwenyewe”.
“Pia kuna baadhi ya watu wamejifunza namna ya kutengeneza hivi vitu kupitia mimi kwaiyo hii nayo ni faida kwangu kwani lengo langu pia nikuona watu wakinufaika kupitia juhudi zangu”,Ameongeza Ranisha.
“Nampongeza sana dada yangu kwa kuamua kufanya kazi hii kwasababu nimejifunza mambo mengi ambayo mwanzoni nilikua sijajui kwani mimi nakaa bweni kwaiyo siku nyingi nakua sipo nyumbani ila kwa kipindi cha mapumziko huwa ananifundisha mfano,kutengeneza keki za miundo mbali mbali pamoja na kuengeneza mchanganyiko wa viungo wa maji ,pia ananipa hamasa ya kutaka kuwa kama yeye”
CHANGAMOTO GANI ANAKUTANA NAZO
Kwakua hakujawahi kutokea kitu kilichokuwa na faida kisha kikakosa kuwa na hasara hivyo basi hata Ranisha ane ankutana na changamoto mbali mabli katika kazi yake ambapoz alisema awali kuna baadhi ya watu walikuwa wakimkatisha tamaa kuwa hatoweza kufankiwa kakini kwasasa anaona mwangaza wa mafanikio kutokana na juhudi anazochukua kukuza kipaji chake pamoja na kuimarisha biashara yake,wakati anaeleza vikwazo anavyokutana navyo katika biashara zake. Rehema amesema,
“ Changamoto kubwa nilizonazo sasa hivi nikukosa sehemu maalumu ya kuafanyia biashara zangu kwani natufanyia nyumbani kwetu,nvifaa pia natumia vya nyumbani na natamani siku moja niwe na vifaa vyangu pamoja na sehemu maalumu ya kufanyia kazi zangu, na wakati mwengine usafiri unanipa shida kwani wakati mwengine nahitaji kupeleka keki kwa mtu lakini nachelewa kupeleka kwasababu usafiri wa daladala na wakati mwengine naipigia boda boda pia anchelewa au anaweza kukukwambia anapeleka mtu kisha atakuja huku wew unachelewa”.
KWANINI BAADHI YA WANAWAKE WANAKATA TAMAA KATIKA KUFANYA BIASHARA
“Wakati tulio nao sasahivi sio wakati wa kukaa majumbani na kuwategemea wanaume ,na washauri wanawake wengu tujitambue na tujaaribu kuangalia kitu gani tunapenda na tunaaidia ya kuanya ambacho ni cha halali hivyo basi tufanye kwani tunajisaidia wenyewe katika mambo yetu madogo madogo kuliko kuwa kila kitu unamtegemea mtu akuletee”,Anasema Rehema
Licha ya kuwa sasa hivi muamko wa wanawake kujishuhulisha na biashara umeongezeka lakini bado baadhi yao hushindwa kujishuhulisha kutokana na sababu tofauti ambazo zinawasababisha kutojishuhulisha kwakufanya biashara, Anna Valentina Subety anaeleza,
”Changamoto ziko nyingi sana ikiwemo kukosa uwezeshwaji na kukosa mashirkiano kwani kuna baadhi ya wanawake wanapenda sana kujituma lakini hawana watu wa kuwawezesha na hata wakijaribu kujiinua wenyewe wanakosa watu wakuwaunga mkono kwa mfano mtu umeolewa na unataka kufanya kazi lakini mume anakukataka usifanye kwasababu tu ya wivu ety ukifanya kazi utakuwa na kiburi au unaweza kuwa na mwaname mwengine au kipato cha mumwe kinakuwa kidogo na muna watoto kidogo inakuwa mtihani, wengine wanazaliwa katika familia maskini kwaiyo hata akitaka kufanya kazi anakosa mtaji kutokana na maisha na wakati mwengine watu wanafuata mambo ya mila”,
”Jamii tunatakiwa kuabadilika kwa kujenga upendo baina yetu, ukimuona mwezako anashida umsaidie kama uanuwezo au hata mawazo tuu, pia wanaume wabadilike na wawaruhusu wake zao wafanye kazi maana wakati mwengine munapoowana munakubaliana vizuri tu ukifika ndani mwanamme anabadili na huduma zenyewe haleti vizuri, kwaiyo mwanaume muache tabia hiyo ili muweze kusaidiana na wake zenu katika majukumu ya familia”,Ameongeza Anna.
WANAUME WANALICHUKULIAJE SUALA LA WANAWAKE KUFANYA KAZI
Kwa kuwa wanawake wengi husema kuwa wanaume ni miongoni mwa sababu zinazowakwamisha hadi kushindwa kufanya kazi,ndipo mwandishi wa Makala hii alipomtafuta mwanaume ili awaelimishe wezake juu ya muhimu wa kuwapa fursa wanawake za kufanya kazi kulingana na maisha ya sasa hivi.Bakari Ali Hamadi anaeleza,
”Tunapo wapa fursa wanawake kufanya kazi kuna umuhimu mkubwa sana hususan katika familia, kwa mfano ikiwa katika familia mwanamke na mwanamme watakuwa wanafanya kazi inakuwa rahisi sana kuwalea watoto wenu kwa kuwapatia elimu bora, pamoja na huduma nyengine na pia wanapata kujifunza kupitia wazazi wao na wao wanakuwa na hamu ya kuataka kusoma kwa bidi ili waweze kuwa kama wao, hata nje ya familia wanawake tunawaona hivi sasa namna wanavyojituma na kufanya kazi kwa uaminifu zaidi kuliko wanaume kwaiyo ni vizuri wanaume kuwaruhkusu wake zao kufanya kazi”.
NANI ATAMUOKOA MWANAMKE
Hata hivyo, miongoni mwa vikwazo kwa wanawake ni kukosa mtaji na uwzeshwaji kwasababu wanawake wengi hajui wapi waelekee pindi wanapotaka kujiajiri kama wajasiriamali ili waweze kujikwamua kiumchumi pamoja na kusaidia familia zao.Lakini zipo taasisi nyingi zenye leongo la kuwainua na kuwawezesha wanawake ikiwemo taasisi ya manamwake TAMWA, TEHAMA na nyenginezo ambazo ni vizuri wanawake kuzitumia ili waweze kupatia msaada wanayostahiki kupewa.
“Sisi tunashuhulikia miradi ya kuwezesha wanawake kiuchumi ambapo mara nyingi tunakuwa tunazingatia mkiradi ya kaya maskini,masuala ya watu wenye ulemavu yaani yale makundi dhaifu ambayo yanakosa fursa katika jamii,kwaiyo tunacofanya tunawaunga katika vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mikopo nafuu isiyo na riba,kwasabu wengi wanakuwa hawana vigezo vya kukopa benki kwaiyo kwaiyo huku kunawasaidia wao kupata mikopo ama mitaji katika biashara zao pia ianwasaidia kuweka akiba ya fedha zao kwani tunajua kuwa wanawake wana mambo mengi mtu anaweza kufanya biashara akapata faida akafanyia mambo yake mengine lakini akiwa na sehemu ya kuweka akiba yake ananyima matumizi yaliyokuwa siyalazima,” Anasema Afisa uwezeshaji wanawake kiuchumi kutoka katika taasisi ya wanawake TAMWA Zanzibar.
Pia katika kuelezea namana wanavyowawezesha wanawake kiuchumi alisema kuwa vikundi hivyo vitawasaidia wanawake kujenga mahusiano na watu tofauti ambao wanaweza kusaidiana katika kuzitangaza biashara zao ,jambo ambalo linaonesha kuwa hakuna sababu ya mwanamke yeyote kukaa nyumbni kwa kisingizio kuwa hana mtaji au amekosa watu wakumsaidia kuweza kufikia malengo yake ikiwa ni pamoja na kujikwamua kiuchumi.
Mwisho.
Comments
Post a Comment