WAKULIMA WASHAURIWA KUTUMIA MBOLEA ASILIA KUTUNZA MAZINGIRA
Na UWEISIYA KHAMIS UNGUJA
WAKULIMA na wamilikk wa mashamba wametakiwa kutumia mbolea Asilia itokanayo na vinyesi,majani makavu,majani ya mjenga uwa ili kuwawezesha kuvuna mazao yenye ubora , inayowawezesha kulinda afya ya mlaji pamoja na kuhifadhi mazingira .
Akizungumza na Mwandishi wa habari hizi Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya Kilimo hai Input Arafa Hamad huko ofisini kwao Mkoa wa kaskazini wilaya ya kaskazini B shehia ya kiomba mvua amesema Utumiaji wa mbolea Asilia ni mbolea yenye faida nyingi kwa mmea kwasababu majani ya mjenga ua yana nitrogen ya kutosha ,samadi ya ngombe ina potassium na nitrogen ambayo inasaidia kulinda afya ya mlaji kwa kuvuna mazao yenye ubora pamoja na kuhifadhi mazingira ,
Aidha amesema kuwa changamoto kubwa ambayo wanakutana nayo ni Uhaba wa soko na uwelewa mdogo wa wakulima juu ya utumiaji wa mbolea asilia .
sambamba na hayo ameeleza jitihada ambazo anazichukua katika kuengeza uelewa wa wakulima juu ya utumiaji wa mbolea asilia amesema kuwa tunaelimisha wanajamii kupitia makongamano mbalimbali kama nane nane ,matamasha ya kibiashara .
Abdi Mbarouk Ameir mfanyakazi wa kampuni hiyo anaeleza namna wanavyonufaika na uwepo wa kampuni hiyo wamesema kuwa Mafanikio ambayo nimeyapata kwanza ni kupata uwelewa wa namna bora ya kutengeneza mbolea asilia.pia amewashauri vijana kutafuta fursa za kuweza kujishuhulisha na sio kukaa tu nyumbani.
Salama Ahmed Salum mfanyakazi wa kampuni hiyo amesema kuwa mafanikio ambayo nimeyapata kipato ambacho nakipata kimenisaidia katika kujikimu matumizi madogo madogo kama vile mahitaji ya nyumbani,kusomeshea watoto,kupata pesa ya kuwanunulia watoto dawa pale ambapo wanaumwa .
Kampuni ya Kilimo hai input company limited ilianza rasmin 2022 inajishuhulisha zaidi na utengenezaji wa mbolea Asilia kauli mbiu inasema Chakula chako Afya yako.
Comments
Post a Comment