HII HAPA SABABU YA DK MZURI MKURUGENZI WA TAMWA ZANZIBAR KUACHA KAZI IKULU.
NA - YUSRA SAID UNGUJA.
MKURUGENZI wa chama cha waandishi wa habari Tanzania TAMWA Zanzibar Dr. Mzuri Issa Amesema Tamwa itaendelea kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili kuhakikisha uwandishi wao unakuwa wa kuleta mabadiliko ya kimaendeleo hasa katika kuonyesha nafasi ya wanawake na uongozi visiwani Zanzibar.
MZURI ISSA ALI- MKURUGENZI TAMWA ZANZIBAR.
Akizungumza na muandishi wa habari hii Mkurugenzi wa chama hicho Dr.Mzuri Issa amesema kwa kipindi kirefu kilichopita nyuma wanawake na wasichana walikuwa hawaandikwi vizuri katika vyombo vya habari jambo ambalo lilikuwa likimpa shida hivyo ameona ni vyema kuwapatia uwelewa waandishi wa habari ili waweze kuonyesha wanawake nafasi na mchango wa wanawake kwa jamii.
Amesema ilifika hatua Watoto na wanawake wanafanyiwa udhalilishaji lakini hakuna mtu wa kuripoti matukio hayo ambapo ilipelekea kuzidi kufanyiwa vitendo hivyo.
Aidha amesema kuwa katika Maisha ya usichana wake alipitia changamoto mbalimbali za kimaisha ambazo zimemtia hamasa ya kujitolea katika kuwasaidia wanawake na watoto wapate haki zao.
Nao baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari Zanzibar akiwemo muandishi mkongwe wa gazeti la habari leo Khatib Suleiman wamesema chama hicho kimekuwa mkombozi mkubwa kwa waandishi wa habari kwani uwandishi wao umekuwa wenye kuleta tija kwa jamii kutokana na mabadiliko yanayojitokeza baada ya kupatiwa mafunzo ya uandishi bora.
Kwa upande wake aliyekuwa Mkurugenzi wa chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania TAMWA Dr. Annanilea Nkya ambae alimshauri Dr. Mzuri Issa kujiunga na taasisi yao amesema ameona uwezo aliokuwa nao katika kutetea haki za wanawake kupitia habari alizokuwa akiandika katika gazeti alilokuwa akifanyia kazi kwa wakati huo lilikuwa likijulikana kwa gazeti la nuru.
Ameongeza kuwa hakuwahi kujutia kumshauri Dr.Mzuri kujiunga na TAMWA kutokana na utendaji kazi wake umekuwa na manufaa mara dufu jambo ambalo limepelekea kwa sasa kuwa na jamii yenye sauti mmoja ya kutetea wanawake na Watoto.
Comments
Post a Comment