VIJANA WAASWA MAMBO HAYA KUFIKIA NAFASI ZA UONGOZI

Na MASSOUD  JUMA - UNGUJA 

VIJANA  wa Zanzibar wanaotarajia kushika nafasi mbalimbali  za uongozi wameshauriwa kujikubalisha kuzikabili changamoto zote ambazo zinatokea katika uongozi na kuwa majasiri katika kutekeleza wajibu wao.

Ushauri huo umetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo bi Fatma Hamad Rajab wakati akizungumzia masuala ya wanawake na uongozi huko ofisini kwake Migombani Zanzibar.

Bi Fatma pia amevitaka vyama vya siasa nchini kuendelea kuwaandaa na kuwapika vijana hasa wa kike ili kuja kuwa viongozi waadilifu, wabunifu na makini na hatimae kuiletea maendeleo Zanzibar.

Nae Mkurugenzi wa taasisi ya Warrior Women Foundation bi Sabra Issa Machano amewataka vijana khasa wa kike wanaotamani kushika nafasi za uongozi wawe tayari kwa kuanza chini kwa kuhudumu katika vyama mbalimbali vya siasa ambavyo wanataka kugombea kwa kutumia uwakilishi wao.

Aidha, Katibu Mkuu wa wizara ya HVUM bi Fatma Rajab ameelezea umuhimu wa wanawake kujishuglisha na kujikomboa kiuchumi huku akisisitiza kuwa wanawake wanatakiwa kujishughulisha na kazi mbalimbali za ujasiriamali  ili kuacha kuwa tegemezi na kuwa na kipato chao wenyewe.

Pia bi Fatma amesema wamefungua kituo maalum kwa ajili ya kuwasaidia vijana kujifunza masuala mbali mbali ya ujasiriamali, uongozi pamoja na afya zao, kituo ambacho kitawasaidia vijana kutokana na tatizo la ajira na kuweza kujiajiri wenyewe.

Akizungumzia kuhusiana na tatizo la mfumo dume, Katibu Mkuu amesema kuwa kwa sasa limepungua kwa kiasi kikubwa kwani kunaonekana kuwepo kwa wanawake wengi kwenye wizara mbali mbali huku akitolea mfano wizara yake ambapo nafasi za uongozi wa juu zimeshikwa na wanawake na wanafanya mambo makubwa na muhimu kwa ustawi wa jamii.

Katika suala hilo la mfumo dume bi Sabra Issa amesema kuwa watu wenye uwezo wa kuuondoa kabisa mfumo dume ni wanawake wenyewe kwani ndio walezi wakubwa na wana njia nyingi za kubadilisha mitazamo hasi dhidi ya wanawake.

Ni muhimu kuimarisha uongozi wa wanawake ili kufikia idadi ya 50/50 kuanzia ngazi za chini hadi katika uongozi wa kitaifa ili zanzibar iwe mfano mkubwa kwa kuwaonesha utendaji mzuri wa wanawake.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI