UFUGAJI WA MAJONGOO BAHARI UNAVYOWANUFAISHA WANAWAKE KIUCHUMI VISIWANI.
Na UWEISIYA KHAMIS- UNGUJA.
ZANZIBAR Ni njrma atakae aje sababu Mengu ni Neema Tupu ii ni baadhi ya misemo ambayo imesikika kwa wingi tangu raisi wa zanzibar wa awamu ya nane aingie madarakani na mmoja kati ya sera ambazo alikuwa anazizungumza sana ni pamoja na suala la UCHUMI WA BULUU ikiwa lengo ni kuinua uchumi wa zanzibar kupitia rasilimali bahari.
"Uchumi wa buluu ni suala jipya katika nchi yetu tafsiri yake ni uchumi endelevu unaotokana na matumizi sahihi ya rasilimali za bahari ,kama ilivyo katika ilani ya Chama Cha Mapinduzi namba 187 ikiieleza uchumi wa buluu na ambao unaweza kuajiri takriban vijana 300,ooo" uchumi wa buluu ni dhana pana yenye kubeba maana nzima ya kutumia rasilimali itokanayo na bahari ikiwemo utalii,uvuvi,kilimo cha mwani,ufugaji wa majongoo bahari ,bandari pamoja na mafuta na gesi. Ndani ya makala hii tutaangalia namna
UFUGAJI WA MAJONGOO BAHARI UNAVYOWANUFAISHA WANAWAKE KIUCHUMI VISIWANI ZANZIBAR, Ufugaji wa majongoo bahari ama hujulikanwa kama sea cucmber ni mmoja kati ya viumbe au fursa zinazopatikanwa baharini ambazo kwa kiasi kikubwa husaidia kuinua pato la taifa au la mtu mmoja mmoja , zanzibar inatajika kuwa ni ya pili katika ukanda wa Afrika kuanzisha ufugaji wa viumbe hai ama majongoo bahari ,kwa upande wa Unguja kuna jumla ya mashamba 44 ya majongoo bahari na kwa upande wa pemba yapo mashamba matano tu ambapo mashamba haya yamejengwa kutokana na fedha za uviko 19 na jumla yalitakiwa yawe mashamba 100 ambapo mashamba 50 unguja na 50 pemba. sehemu zinazofugwa majongoo bahari ni Unguja ukuu kae pwani, Fukuchani, Uzi, Kilimani,Kama,na kwa Pemba yanapatikanwa ukunjwi wete. wakaazi mbalimbali visiwani zanzibar wamehamasika juu ya utumiaji wa rasilimali zinazopatikanwa baharini ikiwemo ufugaji wa majongoo bahari , Makala hii imefunga safari moja kwa moja kuelekea mkoa wa kusini, wilaya ya kusini Unguja Ukuu shehia ya kae pwani lengo ni kutaka kufahamu namna ufugaji huu unavyofanyika na JE mazingira gani ambayo jongoo anafugika vizuri? Mwamvua Othman ni mwanachama wa kikundi cha stahamili anasema " kwanza unanunua mbegu za majongoo bahari alafu unaweka katika shamba lako alafu unasubiri kwa muda wa mwezi mmoja au miezi minane au mwaka alafu unaangalia yakiwa tayari unayavuna, lakini pia unaweza kukaa baada ya mwezi unaangalia ambalo lipo tayari unavuna" Ameongeza kwa kusema " mazingira anayofugika vizuri jonngoo ni sehemu yenye mchanga mchanga ,isiwe na tope nyingi na isiwe sehemu yenye magangari mengi " Makala hii haijaishia hapo tu imefunga safari na kuelekea Mkoa wa Mjini Magharibi,Wilaya ya Mjini kukutana na jumuia ya wakulima hai inayopatikanwa kilimani mmoja kati ya jumuia ambazo zinajishuhulisha na ufugaji wa majongoo bahari,pamoja na kaa na kukutana na Daudi M uhammed Salum ambae ni Mwenyekiti wa jumuia hiyo, anatueleza namna majongoo hayo yanavyofugwa kitaalam, Je majongoo hayo yanafaida gani ndani ya mwili wa binadamu? Je ni changamoto zipi ambazo wanakutana nazo na wanazitatua vipi? UFUGAJI WAKE "jongoo anafugwa katika maji madogo ambayo ni sentimeter 10 yenye topetope kwasababu jongoo hataki joto,tafiti zimeonyesha kuwa asilimia 80 jongoo anafugika vizuri Unguja na Pemba na aina hii ya jongoo ni rahisi sana kufugika kwasababu ufugaji wake unafanyika maji yakiwa kidogo, Jongoo huyu mweupe anakula vitu vinavyopatikanwa baharini kama vile majani, bacteria wadogo ,vitu vilivyooza, na vifaa vinavyohitajika ni nyavu maalum,na vyuma visivyoota kutu," Ameongeza kwa kueleza mazingira ambayo jongoo anafugwa " kujengwa shamba la ukubwa wa mita 40 kwa 40 au zaidi, sehemu yenyewe iwe haina matumizi ya shuhuli nyengine za baharini, iwe na rutuba na isiwe na changamoto yoyote kama mawimbi makali au kutumika kama bandari" KUSARIFU " Baada ya kuwavuna majongoo unawatoa matumbo,unawachemsha kwa dakika 15 alafu unawaacha watoke maji,baada ya hapo unawaweka kwenye ndoo yenye chumvi ya madonge alafu unawahifadhi kwa muda wa siku tano mpaka wiki moja, unawatoa na kuwachemsha tena kwa dakika 15 huku unawakoroga baada ya hapo unamuosha kwa maji safi pamoja na kumtoa calcium kwa kutumia majani ya mpapai au magamba ya kaa na baada ya hapo unamuanika na hatua ya mwisho ni kumuandaa kwaajili ya kusafirisha bidhaa hiyo." FAIDA ZA MAJONGOO BAHARI KIAFYA. "Jongoo anasaidia kufanya ngozi kuwa nyororo,kukuza nywele,anasaidia katika kuengeza wingi wa maziwa kwa mama wanaonyonyesha., anasaidia kuponesha utokaji wa damu kwenye ufizi, anasaidia kuondosha kovu,anasaidiya kuponesha maradhi ya kensa kwa asilimia 85 pamoja na kuondoa maumivu ya viungo lakini pia kwa akina baba anasaidia kuengeza nguvu za kiume." CHANGAMOTO. "Changamoto ambayo tunakutana nayo ni wizi wa majongoo,maradhi ya kubabuka kwa ngozi,watu wengi hawapo tayari ." NAMNA AMBAVYO WANATATUA CHANGAMOTO HIZO. "Kujenga kwa kibanda ambacho kinasaidia katika suala zima la ulinzi wa mazao hayo ,pamoja na kuhamasisha wananchi katika eneo husika la ujenzi ili kusaidia katika suala la ulinzi." Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 30 ya uchumi wa zanzibar unategemea bahari na asilimia 81 ya wanaofanya shuhuli hizo ni wanawake mwandishi wa makala hii amekutana ana kwa ana na wanawake wa shehia ya kae pwani Unguja ukuu wanaojishuhulisha na ufugaji wa majongoo bahari na wanawake hao wanaeleza hali ya maisha ilivyokuwa kabla na baada ya kufanya biashara hiyo. Husna Busara Hassan " Hapo awali maisha yalikuwa ni magumu sana ,kipato kilikuwa ni cha shida mahitaji ya nyumbani yalikuwa ni magumu kiasi cha kukosa pesa ya kumsomeshea mtoto.” Ameendelea kwa kueleza hali jinsi ilivyosasa “Mafanikio ambayo nimeyapata kupitia shuhuli zangu hizi ni kusomesha watoto wangu, kujenga nyumba yangu, kununua matumizi madogo madogo ya nyumbani", Mwamvua Othman”zamani maisha yalikuwa ni ya shida,kupata fedha ya kuendesha familia ilikuwa ni ngumu kiasi cha kukosa pesa ya kununua mahitaji ya nyumbani.” Ameongeza kwa kusema hali ilivyosasa " nimepata pesa za kuwashuhulikia familia yangu, kujenga nyumba, " Wanunuzi wakubwa wa bidhaa hizi ni wachina,vietnam,taiwan,canada. JE soko la bidhaa hii lipoje? Fadhil Haji Juma, mfugaji wa majongoo bahari anasema"soko la majongoo bahari lipo lakini halina uhakika ambapo jongoo namba 1 ambao ni wabichi wanaweza kuuzwa hamsini elfu, namba 2 anauzwa thelathini na tano mpaka arobaini na namba 3 anauzwa kati ya ishirini mapaka ishirini na tano elfu, ila mazingira ya soko hayapo sawa na hayapo wazi. Daudi muhammed "soko la jongoo mkavu k anaweza kuuzwa laki mbili ,laki tatu inategemea na wingi wa majongoo" Makala hii inatuonesha namna wanawake wanavyopambana na kuhakikisha wanachangia japo kidogo katika ujenzi na ustawi wa familia, na hadi hapa ndio tunafikia mwisho wa makala hii
Comments
Post a Comment