BI ABEDA ASHAJIHISHA ELIMU YA WATU WAZIMA KATIKA SHEHIA YA KITOPE.
Na RAIFFA ABDALLAH UNGUJA
MKUFUNZI wa elimu ya watu wazima Abeda khamis Mohamed, amehimiza jamii kuyapa umuhimu masomo ya watu wazima ili waweze kujihudumia.
Bi Abeda ameyasema hayo wakati akingumza na Mwandishi wa habari hizi huko katika shehia ya kitope, wilaya ya Kaskazini B, mkoa wa kaskazini Unguja.
Amesema lengo la kuyaanzisha masomo hayo ni kuwasaidia watu ambao hawakubahatika kupata elimu katika enzi zao za utotoni jambo ambalo linawafanya kupitia wakati mgumu sana kwani elimu ndio kila kitu katika maisha ya leo.
Hata hivyo amesema , elimu hiyo itawawezesha watu kujuwa kuandika na kusoma kwani hii itafanya wawe na uelewa mzuri wa mambo ambayo yanatokea katika jamii na kuwawezesha kutoka michango ya kimawazo wakati ukihitajika.
" watu walio wengi hawajui hata kuandika majina yao na ukiwambiya waje kusoma wanakuwa hawajitokezi , darasa la kusoma watu 15 lina wanafunzi 6 na wengi wamesajili majina yao lakini hawahudhurii darasani."
Sheha wa shehia ya kitope bwana Ramadhan Saidi Abdallah, amekiri kuwepo kwa elimu ya watu wa zima katika shehia yake na kushauri watu kujitokeza kwa wingi na wasipuuze fursa hii adimu kwani elimu ndio itakayowafanya wao waweze kupata kuongoza vizuri familia na hata jamii ili kuweza kuleta maendeleo katika jamii yao.
"Mimi nimepata nafasi yangu ya Usheha kutoka na elimu yangu niliyokuwa nayo kwani nilionekana nitaweza kukabili matatizo ya wanakijiji wangu na kuyasemea na au kuandika baruwa na kufikisha sehemu husika ." Alisema sheha huyo.
Amesema elimu itatoa muongozo wa maisha kwa mtu binafsi na kufanya awe na uwezo wa kujuwa kitu gani wafanye wakati anapokabiliwa na matatizo au kutaka kufanikisha vitu vya maendeleo kama kujenga , kusomesha mtoto na hata kusimamia familia.
Aidha aliwataka Wanakijiji kutoa ushirikiano kwa mwalimu huyo BI Abeda na kwenda kusoma kwani wanafunzi watakapohudhuria vizuri walimu huyo atakuwa na ari zaidi ya kusomesha na kufikia malengo ya kuazisha elimu hiyo ya watu wazima.
Baadhi ya wanakijiji wa kijiji cha kitope ambao pia ni wanafunzi wa Elimu ya watu wazima , Kazija Mussa na Hija Khamis wamesema, watajitahidi waweze kuhudhuria na kusoma kwa bidii na kuomba baadhi ya wezao waweze kufahamishwa zaidi kuhusu mafunzo hayo maana walio wengi wezango uwelewa ni mdogo sana.
Comments
Post a Comment