Tume kurekebisha Sheria yaahidi Mabadiliko kufikia usawa wa kijinsia katika Uongozi.
NA ASIA MWALIM- UNGUJA TUME ya Kurekebisha sheria Zanzibar, imesema itashirikisha na Tume ya Sheria Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika kuzifanyia mapitio sheria zisizo zingatia jinsia katika ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi . Katibu wa Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar, Mussa Kombo Bakari, aliyasema hayo wakati wa semina ya majadiliano ya sheria yaliandaliwa na shirika la Women in Law and Development Africa (WILDAF), huko Beach Resort Mazizini Unguja. Alisema tume hizo kwa pamoja zitazingatia suala la wanawake wakati wa kufanya mapitio ya sheria ya vyama vya siasa na sheria ya taifa ya uchaguzi, ili kuona kundi hilo linakua mstari wa mbele. Aidha alisema lengo la semina hiyo ni kujenga uwezo wanasheria ili wapate kuwakisi masuala ya wanawake wakati wa kuzipitia sheria, hatimae kutoa miongozo mizuri kwa makundi yote. Katibu Mussa, alifahamisha kuwa, sheria za awali zilishindwa kuzingatia jinsia, ni muhimu kujenga uele...