WAANDISHI WA HABARI TAIFA LINAWASIKILIZA SANA TUMIENI FURSA HII KUSAIDIA MAKUNDI YALIOSAHAULIKA KATIKA KUSEMEA CHANGAMOTO ZAO ZIPATE UFUMBUZI.
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA
"TUNGEPENDA kuona kesi Za udhalilishaji kwanza Kila Mwaka zinapungua, hatutaki kabisa kudhalilishwa,wanawake, watoto na watu wenye Ulemavu ,Tuangalie ukuaji na Uwajibikaji wa Vyombo vinavyosimamia Sheria, kwa sababu Mwandishi wa Habari anaweza kufuatalia mlolongo mzima wa kesi mwanzo hadi mwisho na jamii ikaweza kuelewa, Bado kuna malalamiko katika masuala ya utolewaji wa hukumu baadhi ya watu wanakuwa huru huku jamii ikijiuliza masuali yanayokosa majibu hivyo waandishi tuyaone haya katika kuandika habari zetu".
Ni kauli ya Mkurugenzi Chama Cha waandishi wa Habari Wanawake Zanzibar Tamwa Dk Mzuri Issa Ali Alipokuwa Akifungua Mafuzo ya siku mbili kwa Waandishi wa Habari wa vyombo mbali mbali Unguja na Pemba kwa njia ya Zoom juu ya haki za makundi yaliyotengwa ikiwa ni pamoja na watu wenye Ulemavu, ushirikishwaji wa wanawake na vijana na wajibu wao wa kutetea mapitio au uanzishwaji wa sheria zinazohusiana na udhalilishaji wa kijinsia na kushawishi utekelezaji wa sheria na sera zinazoshughulikia mahitaji ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu Mapema leo Asubuhi.
Alisema kuwa waandishi ndio ambao wanauwezo Mkubwa wa kushawishi upatikanaji wa haki mbali mbali kupitia kalamu zao kuona Tatizo la udhalilishaji haliongezeki Visiwani Zanzibar, pamoja na kuzisemea ili ziweze kupatiwa ufumbuzi Chanagamoto za Makundi ya vijana wanwake na watu wenye ulemavu na kuweza kudai haki zao kwa lengo la kuondokana na Udhalilishaji.
Dk Mzuri Issa Ali - Mkurugenzi Tamwa Zanzibar
Akizungumza na waandishi kwa upande wa kisiwani Pemba mratibu wa chama hicho Fat-hiya Mussa Said Amesema lengo La Mafunzo hayo ni kufanyia kazi changamoto mbali mbali ziakazoibuliwa na kuzifanyia uchechemuzi na kuona kunakuwa na Sheria moja ya udhalilishaji au kuona marekwbisho katika sheria zilizopo, pamoja na kuhamaisha utekelezwaji wa Sheria, Ushiriki na ushirikishwaji wa wanawake, vijana pamoja na watu wenye ulemavu katika kupata fursa sawa za kimaendeleo.
Fat- hiya Mussa Said- Mratibu Tamwa Pemba.
Mkutano huo Ulioandaliwa na Tamwa Zanzibar kwa waandishi wa habari Unguja na Pemba Ni katika utekelezaji wa mradi wa Kuhamasisha Hatua za Kitaifa dhidi ya Vitendo vya udhalilishaji Zanzibar unaotekelezwa na Tamwa Zanzibar kwa kushirikiana na Foundation for Civil Society ambapo katika mkutano huo Mada mbali mbali ziliwasilishwa zilizohusu masuala yanayigusa makundi hayo.
Mwisho
Comments
Post a Comment