59 Ya Mapinduzi Neema zinaonekana

NA FATMA SULEIMAN - PEMBA. 

WAZIRI wa Ardhi na Maendeleo ya Makaazi Mh. Rahma Kassim Ali amewaagiza wapiganaji wa kikosi cha kuzuia magendo (KMKM) kuimarisha ulinzi wa usafirishaji wa magendo ya karafuu ili kudhibiti uchumi wa nchi.

Waziri Rahma ametowa agizo hilo wakati akizungumza na wapiganaji wa kikosi cha KMKM, viongozi wa chama na serikali na wananchi wa shehia ya Gando, baada ya kuweka jiwe la msingi mradi wa kambi ya KMKM Gando akiwa katika muendelezo wa shamra shamra za kuadhimisha miaka 59 ya mapinduzi ya Zanzibar.
Amesema lengo la kukombolewa kwa wazanzibar ni kuhakikisha wananchi wanafaidika na huduma za kijamii bila ya ubaguzi, ambapo kwa sasa serikali inategemea zao la karafuu kupata fedha za kigeni kutekeleza miradi ya kimaendeleo.

Akitowa salamu za mkoa Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Mh. Salama Mbarouk Khatib amewashukuru wananchi wa Gando kutowa ardhi yao kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kambi hiyo.

Akisoma taarifa ya kitaalamu ya mradi huo Katibu Mkuu wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Idara Maalumu za SMZ Issa Mahfoudh Haji amesema mradi huo unajumuisha ujenzi wa kituo cha afya, hanga, kota gadi na ofisi ya mkuu wa kambi,ambao utaondosha usumbufu wa makaazi kwa wapiganaji. 

Kwa upande wake Mkuu wa KMKM Kamandi ya Pemba kamanda Omar Ali Mussa amesema kukamilika kwa mradi ikiwemo kituo cha afya itsaidia upatikanaji wa matibabu bora kwa wapiganaji na maafisa pamoja na wananchi kwa wakati.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI